12 Februari 2026
Korea Kaskazini ipo katika mchakato wa kumuandaa Kim Ju-ae, binti wa Kim Jong Un, kama kiongozi ajaye wa taifa hilo.
Idara ya Kijasusi ya Korea Kusini (NIS) ilisambaza taarifa ya mchakato huo, wakati wa mkutano wa ndani wa bunge la nchi hiyo, kulingana na Park Sun-won na Lee Seong-kweun, wabunge kutoka bunge la Korea Kusini.
Hata hivyo, serikali ya Korea Kaskazini haikusema chochote kuhusiana na madai hayo.
Ju-ae amekuwa akionekana hadharani katika matukio makubwa ya Korea Kaskazini, ikiwemo sherehe za Jeshi la Wananchi la Korea Kaskazini na ziara yake katika eneo la Kumsusan, ambao imhifadhiwa miili ya Kim Il Sung na Kim Jong Il, ambao ni viongozi wa zamani wa taifa hilo.
CHANZO:AA











