| Swahili
AFRIKA
2 dk kusoma
Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika aeleza wasiwasi wake kuhusu kuongezeka kwa uhasama jimbo la Tigray
Mahmoud Ali Youssouf ametaka kuwepo kwa utulivu, na kuonya dhidi ya kukiuka makubaliano ya amani ya Pretoria ya 2022 huku kukiwa na wito wa kuepuka mapigano eneo la Tigray
Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika aeleza wasiwasi wake kuhusu kuongezeka kwa uhasama jimbo la Tigray
Mwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika Mahmoud Ali Youssouf./ AA
30 Januari 2026

Mwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika (AU) Mahmoud Ali Youssouf siku ya Ijumaa alitoa wito wa “kuwepo kwa utulivu” kufuatai taarifa za vyombo vya habari za kusitishwa kwa safari za ndege na kuongezeka kwa uhasama eneo na kaskazini mwa Ethiopia la Tigray.

Wasiwasi wa mkuu huyo wa AU unakuja huku kukiwa na wito kutoka kwa wanaharakati na vyama vya kisiasa huko Tigray kuepuka kurudi tena kwa mgogoro.

Katika barua ya wazi, Salsay Woyane, chama cha upinzani kinachoendesha harakati zake kwenye eneo hilo, kikionya wapatanishi wa kimataifa kuhusu “kuporomoka kabisa” kwa hali tete ya amani ya Tigray.

Chama hicho kimetoa wito wa kuwepo kwa mazungumzo ya kidiplomasia kati ya serikali kuu ya Ethiopia na chama cha Tigray People’s Liberation Front kuepuka kile wanachokitaja kuwa “hali ya hatari inayoweza kuepukika.”

Vyombo vya habari vinaripoti kuwa hali ya usalama ilibadilika siku ya Alhamisi baada ya shirika la ndege la Ethiopian Airlines ghafla kusitisha safari zake zote katika mji mkuu wa eneo hilo Mekelle, pamoja na miji ya Axum, Shire na Humera, wakitaja “hali isiyoweza kuepukika.”

Ripoti hiyo pia inaeleza kuhusu mapigano mengine katika eneo la Tselemti za magharibi mwa Tigray, eneo tete kiusalama tangu kumalizika kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe.

“Mwenyekiti anatoa wito kwa pande zote kuwa watulivu, kujizuia na hali yoyote ambayo itazua hofu, na kutatua masuala yote kwa njia ya majadiliano yenye tija, kwa kuzingatia majukumu na lengo kwa kuzingatia makubaliano ya COHA,” AU ilisema katika taarifa.

Uhasama uliopo sasa unaonesha changamoto kubwa kwa makubaliano ya COHA, yaliyotiwa saini mjini Pretoria mwezi Novemba 2022.

CHANZO:AA