Ghana yafanya uchunguzi wa kitaifa kuhusu madai ya plastiki katika chipsi za ndizi

Msimamizi alisema kuwa wanafanya kazi pamoja na mamlaka za ndani na Polisi wa Ghana ili kufuatilia wachuuzi.

By
Katika taarifa iliyotolewa na FDA, imesema uchunguzi ulilenga kubaini ukweli wa madai hayo na kuwalinda walaji. / Others

Ghana imeanzisha uchunguzi wa kitaifa kuhusu tuhuma za kuchanganywa plastiki katika 'chips' za ndizi zinazouzwa nchini humo.

Mamlaka ya Chakula na Dawa (FDA) imesema imeanza kufuatilia bidhaa hiyo sokoni na kufanya vipimo vya maabara nchi nzima baada ya video iliysambaa katika mitandao ya kijamii inayoonesha waandaaji wa ndizi kwa makusudi wakiyeyusha plastiki katika mafuta ya moto wakati wa uandaaji kwa lengo la kuongeza wingi wa bidhaa hiyo lakini pia kurefusha muda wa kuharibika, kwa mujibu wa Wakala wa Habari Ghana.

Katika taarifa iliyotolewa na FDA, imesema uchunguzi ulilenga kubaini ukweli wa madai hayo na kuwalinda walaji.

"Kwa rekodi, kuyayusha plastiki kwa makusudi katika mafuta yanayochemka ni uharibifu wa moja kwa moja wa chakula, na kukifanya kutofaa kwa matumizi ya binadamu," imesema Mamlaka hiyo.

FDA imeonya kwamba bidhaa za plastiki, hasa mifuko katika mafuta ya moto, ni hatari kwa afya na kutoa sumu iliyopo kwenye plastiki na kuingia kwenye chakula," imesema.

Mamlaka imesema inashirikiana na mamlaka ya ndani na Polisi wa Ghana kufuatilia wachuuzi wanaoshukiwa na kuahidi kutoa matokeo ya uchunguzi pindi yatakapokamilika.

Kesi za chakula kuwa na sumu zimekuwepo siku za nyuma na zimehusishwa na chakula cha barabarani, maji machafu na kutokuwepo kwa sheria madhubuti.

Mwaka 2022, FDA ilifunga mgahawa maarufu baada ya kuwepo kwa taarifa za wateja kula chakula chenye madhara.