Katika sehemu moja ya mji wa Freetown, mikono ya Mariama inatetemeka, kutokana na kupiga deki na kufua kwa muda mrefu.
Aliahidiwa maisha mazuri kama msusi nchini Saudi Arabia, badala yake akajikuta amekwama katika sehemu moja, akifanya kazi saa 19 kwa siku katika familia ya watu 12.
"Hawakunipa chakula cha kutosha," Mariama aliielezea TRT Afrika, akiwa bado ana maumivu. "Nilikuwa nakula tu kwa sababu nawapikia."
Siyo Mariama pekee anaepitia hali hii. Kote Afrika Magharibi, mamilioni ya wafanyakazi wa nyumbani wanateseka katika majumba, mchango wao hautambuliki, haki zao hazizingatiwi.
Nchini Kenya, mfanyakazi mwingine wa nyumbani, Grace*, anafahamu vizuri kuhusu hali hii. Alianza kufanya kazi ya nyumbani akiwa na umri wa miaka 14 baada ya wazazi wake kufariki, alifanya kazi katika familia ya kitajiri jijini Nairobi kwa miaka mitatu bila kupumzika hata siku moja.
"Sikuwa nalipwa kwa wakati, na nilipouliza kuhusu mshahara, walikuwa wananiambia kuwa nina bahati kupata sehemu ya kulala," alikumbuka. Sauti yake inatetemeka akieleza namna alivyofungiwa ndani ya nyumba wakati familia hiyo ilipokuwa inaenda likizo, akiachwa bila chakula. Nchini Kenya, kama ilivyo maeneo mengine ya Afrika, wafanyakazi wa nyumbani hupewa jina la tafsida "mameneja wa nyumbani" au "wasaidizi"—majina ya sifa ambayo huficha madhila wanayopitia watu na kukwepa uwajibikaji wa kisheria.
Kulinda upatikanaji wa ajira
Huku Marx Conteh, Katibu Mkuu wa Chama cha Wafanyakazi nchini Sierra Leone, akionya kuhusu, "Hatua ya kutoka katika uidhinishaji hadi utekelezaji ni ndefu na inahitaji watu kushirikiana zaidi. Wakaguzi wa taratibu za kazi ndiyo wanaotakiwa kulinda kwa kuhakikisha kuwa sheria za kazi zinaheshimiwa, na utekelezaji thabiti. la sivyo kuna hatari ya kuwa maneno tu bila utendaji."
Kwa maelfu ya wafanyakazi wa nyumbani, mabadiliko haya yanatakiwa kuwa zaidi ya mabadiliko ya kisheria. Yanaashiria katika kuelekea kulinda ajira, kutambuliwa, na imani kuwa haki zao zitaheshimiwa. Kwa kuangazia mazingira bora ya ustawi wa jamii, mikataba ya ajira, na mifumo ilioimarishwa ya kuwasilisha malalamiko, Sierra Leone inajitahidi kutengeneza mfumo ambapo wafanyakazi wa nyumbani watakuwa wanawezeshwa—siyo kunyanyaswa.
Na huku Sierra Leone ikiendelea na mabadiliko hayo, kufanya utashi wa kisiasa kuwa uhalisia kwa wafanyakazi wake ambao haki zao za msingi hazizingatiwi, dira ya mustakabali wa haki inaibuka.
Alma Heroe, Mkurugenzi Mkuu wa Chama cha Wafanyakazi wa Nyumbani cha Sierra Leone, anasisitiza kuhusu umuhimu wa kuwalinda wafanyakazi wa nyumbani.
"Tudhamirie kwa pamoja kuhusu kujenga mifumo inayofanya kazi za nyumbani kuwa chanzo cha kuwawezeshwa —siyo kuwanyanyasa," Heroe anaeleza.
Ni dira ambayo inatoa matumaini kwa Mariama, Grace, na wengine wengi kwamba kazi zao zitalindwa kwa heshima na taadhima kama wanavyotarajia.
*Majina yamebadilishwa kulinda wahusika kutotambuliwa





















