| Swahili
UTURUKI
2 dk kusoma
Njia ya nne ya kurukia ndege uwanja wa Istanbul kukuza uchukuzi, asema Rais Erdogan
Kulingana na Erdogan, ndani ya miaka 24 ya uongozi wa chama cha AK, shughuli ndani ya uwanja huo zimeongezeka mara mbili, kutoka 26 hadi mara 58.
Njia ya nne ya kurukia ndege uwanja wa Istanbul kukuza uchukuzi, asema Rais Erdogan
Rais Recep Tayyip Erdogan wa Uturuki./Picha:AA

Rais Recep Tayyip Erdogan wa Uturuki, amebainisha kuwa njia ya nne ya kurukia ndege ya uwanja wa ndege wa Istanbul, una mchango mkubwa katika sekta ya kimataifa ya uchukuzi.

“Kwa jiji la Istanbul pekee, tumeingiza kiasi cha Lira trilioni 2.12 katika uwekezaji wa usafiri na miundombinu katika sekta ya usafiri wa anga,” alisema Erdogan wakati wa ufunguzi wa njia hiyo siku ya Ijumaa.

Kulingana na Erdogan, ndani ya miaka 24 ya uongozi wa chama cha AK, shughuli ndani ya uwanja huo zimeongezeka mara mbili, kutoka 26 hadi mara 58.

"Kwa pamoja, tumeifanya Uturuki iwe na nguvu na heshima ulimwenguni kote," alieleza.

Kiongozi huyo, aliongeza kuwa Uturuki itaendelea kuwekeza ili kuufanya uwanja wa Istanbul uendelee kung’aa kimataifa.

Kulingana na Erdogan, mwezi uliopita, uwanja huo ulivunja rekodi kwa kupokea ndege 1,787, idadi kubwa zaidi Uturuki na Ulaya kwa ujumla.

 “Waliwahi kusema kuwa ndege haztoruka kutoka hapa, lakini ndani ya siku moja tulishuhudia ndege 1,787 zikiruka na kutua ndani ya siku moja,” alisema.

Katika hafla hiyo ya Ijumaa, Erdogan alizindua njia hiyo ya zege, yenye urefu wa mita 2,820 yenye thamani ya Dola bilioni 1.05 na kufanya idadi za kurukia ndege kufikia sita, zikiwemo njia kuu nne.

Erdogan aliongeza kuwa, Uturuki imewekeza Lira trilioni 2.12 kwa ajili ya miundombinu ya sekta ya anga.

 

CHANZO:Anadolu Agency