tokea masaa 8
Aliyekuwa Askofu wa Jimbo Katoliki la Kondoa nchini Tanzania, Bernardin Francis Mfumbusa amefariki dunia.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC), Askofu Mfumbusa amefariki dunia Aprili 14, 2026 katika Hospitali ya Benjamin Mkapa, Dodoma, alipokuwa akipatiwa matibabu ya dharura.
ZILIZOPENDEKEZWA
Itakumbukwa kwamba, Aprili 9, 2026 Baba Mtakatifu Leo XIV alikuwa amemteua Askofu Bernardin Francis Mfumbusa, Rais wa Kamati ya Mawasiliano ya Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu Afrika na Madagascar, “Pan African Episcopal Conference For Social Communication, CEPACS,” kuwa ni Mjumbe wa Baraza la Kipapa la Mawasilianiano ya Jamii.
“Kanisa limempoteza Askofu na mtaalam mbobezi wa Mawasiliano ya Jamii,” ilisema taarifa iliyotolewa na TEC.
CHANZO:TRT Afrika Swahili











