6 Februari 2026
Shirikisho la Soka la Morocco (FRMF) limekanusha vikali taarifa zinazosambaa mitandaoni zikidai kuwa kocha wa timu ya taifa, Walid Regragui, ametoa pendekezo la kujiuzulu kufuatia kipigo cha fainali ya AFCON dhidi ya Senegal.
FRMF imesisitiza kuwa taarifa hizo si za kweli na kwamba Regragui bado yuko kazini na ataendelea kuiongoza timu ya taifa.
Katika taarifa rasmi, FRMF ilisema: "Habari hizi zinazozunguka mitandaoni hazina msingi wowote. Kocha Walid Regragui bado yupo kazini na ataendelea kuiongoza timu ya taifa."
Haya yanajiri miezi kadhaa tu kabla ya kuanza kwa Kombe la Dunia, jambo linalowafanya mashabiki wengi kufuatilia kwa karibu mustakabali wa benchi la ufundi la simba wa Atlas.
CHANZO:TRT Afrika














