Shirikisho la Soka la Morocco lakana taarifa za kujiuzulu kwa kocha

Taarifa zimesambaa katika mitandao ya kijamii ya kuwa kocha wa timu ya taifa ya Morocco, Walid Regragui amependekeza kujiuzulu.

By Mustafa Abdulkadir
Kocha wa timu ya taifa ya Morocco, Walid Regragui aliipeleka timu hiyo nusu fainali katika michuano ya Kombe la Dunia 2022. / / Reuters

Shirikisho la Soka la Morocco (FRMF) limekanusha vikali taarifa zinazosambaa mitandaoni zikidai kuwa kocha wa timu ya taifa, Walid Regragui, ametoa pendekezo la kujiuzulu kufuatia kipigo cha fainali ya AFCON dhidi ya Senegal.

FRMF imesisitiza kuwa taarifa hizo si za kweli na kwamba Regragui bado yuko kazini na ataendelea kuiongoza timu ya taifa.

Katika taarifa rasmi, FRMF ilisema: "Habari hizi zinazozunguka mitandaoni hazina msingi wowote. Kocha Walid Regragui bado yupo kazini na ataendelea kuiongoza timu ya taifa."

Haya yanajiri miezi kadhaa tu kabla ya kuanza kwa Kombe la Dunia, jambo linalowafanya mashabiki wengi kufuatilia kwa karibu mustakabali wa benchi la ufundi la simba wa Atlas.