| Swahili
ULIMWENGU
2 dk kusoma
Iran yadai wanajeshi 500 wa Marekani wameuawa ndani ya siku tano za vita
Marekani imetangaza vifo vya wanajeshi sita pekee tangu Jumamosi, wanne kati yao kutoka nchini Kuwait.
Iran yadai wanajeshi 500 wa Marekani wameuawa ndani ya siku tano za vita
Ali Larijani ameapa Iran kulipiza kisasa kufuatia kifo cha kiongozi wake mkuu Ali Khamenei. / Reuters
5 Machi 2026

Afisa wa ngazi ya juu wa ulinzi wa Iran, Ali Larijani, Jumatano amedai kuwa zaidi ya wanajeshi 500 wa Marekani wameuawa katika mapigano yanayoendelea.

Katika ukurasa wa X, Larijani amemlaumu Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu kwa kuwaingiza Wamarekani katika vita na Iran.

"Hivi sasa lazima apige hesabu — huku kukiwa na zaidi ya wanajeshi wa Marekani 500 waliouawa katika siku chache zilizopita, je Marekani bado ni ya kwanza- au Israel," aliandika.

Marekani imetangaza vifo vya wanajeshi sita pekee tangu Jumamosi, wanne kati yao kutoka nchini Kuwait.

Larijani, ambae awali alikuwa mshauri mwandamizi wa Khamenei NA hivi sasa mkuu wa Baraza la Ulinzi wa Taifa la Iran, ametahadharisha kwamba, "simulizi bado inaendelea."

“Kuuawa akiwa shahidi kwa Imam Khamenei malipo yake itakuwa ni makubwa kwenu. Mungu akipenda,” amesema.

Kauli yake inakuja huku mapigano kati ya Iran na Marekani yakiendelea kuongezeka.

Mapigano yalianza kwa mashambulizi ya pamoja kati ya Marekani na Israel dhidi ya Iran Jumamosi, na kusababisha mauaji ya Kiongozi Mkuu wa Iran Ali Khamenei, pamoja na viongozi wengine waandamizi katika jeshi ambao walishika nafasi hizo kufuatia kuuliwa kwa warithi wao na Israel mwezi Juni, 2025.

Takriban Wairan 1,050 wameuawa ndani ya siku nne ya mapigano, kwa mujibu wa serikali, ikiwemo wanafunzi 165 kusini mwa mji wa Minab, na kuibua hasira kali.

Khamenei alilengwa akiwa katika makazi yake jijini Tehran akiwa pamoja na familia yake, ikiwemo mke wake, binti yake, mke wa mtoto wake, mkwe wake na wajukuu zake.

Uongozi wa Iran umeapa kulipiza kisasi kwa mauaji hayo huku wakituma makombora na ndege zisizo na rubani kuishambulia Israel na kambi za Marekani zilzopo Mashariki ya Kati.

Katika taarifa ya Jumatatu, Larijani amesema kuwa Iran "imejiandaa kwa vita vya muda mrefu.

Pia amekataa pendekezo la majadiliano na Marekani kama ilivyopendekezwa na Waziri wa Mamboy ya Nje wa Oman Badr Al Busaidi, ambae alisimamia mazungumzo ya awali ambayo hayakuwa ya moja kwa moja kati ya pande mbili kabla ya kuanza kwa mapigano.