| Swahili
UTURUKI
2 dk kusoma
Rais Erdogan, aisifia Ukanda wa Kati kuwa ‘Barabara ya Silki ya kisasa’ katika ziara yake Kazakhstan
“Tunataka kusafirisha kiasi kikubwa zaidi cha mafuta kutoka Kazakhstan, moja ya nchi zinaozoongoza duniani kwa kuuza mafuta ghafi duniani, kwenda kwenye masoko ya kimataifa kupitia nchi yetu,” alisema rais wa Uturuki.
Rais Erdogan, aisifia Ukanda wa Kati kuwa ‘Barabara ya Silki ya kisasa’ katika ziara yake Kazakhstan
Erdogan alitoa matamshi hayo huko Kazakhstan, ambapo alipokelewa na Rais Kassym-Jomart Tokayev katika sherehe rasmi huko Astana. / / AA

Rais wa Uturuki, Recep Tayyip Erdogan, siku ya Alhamisi alisisitiza umuhimu wa Ukanda wa Kati wa Mashariki-Magharibi unaopita Bahari ya Caspian, akiuita “sawa na Barabara ya Silki ya kisasa.”

Katika mkutano na waandishi wa habari nchini Kazakhstan, Erdogan alisema umuhimu wa ukanda huo unaendelea kueleweka zaidi kila siku inapopita.

Aliahidi kwamba Uturuki itaendelea kuutangaza ukanda huo pamoja na Kazakhstan na washirika wengine kwa ajili ya usafirishaji wa mizigo na rasilimali za nishati kwenda nchi za Magharibi.

“Tunataka kusafirisha kiasi kikubwa zaidi cha mafuta kutoka Kazakhstan, moja ya nchi zinaozoongoza duniani kwa kuuza mafuta ghafi duniani, kwenda kwenye masoko ya kimataifa kupitia nchi yetu,” aliongeza.

Erdogan alitoa kauli hizo akiwa Kazakhstan, ambako alipokelewa na Rais Kassym-Jomart Tokayev katika sherehe rasmi jijini Astana.

Baada ya sherehe ya mapokezi na utambulisho wa wajumbe wa pande zote mbili, viongozi hao walifanya mazungumzo ya faragha, na baadaye wakaongoza kwa pamoja mkutano wa sita wa Baraza la Ushirikiano wa Kimkakati wa Ngazi ya Juu kati ya Uturuki na Kazakhstan.

Katika ziara hiyo, Tokayev alimkabidhi Erdogan tuzo ya heshima “ Nishani ya Khoja Ahmed Yasawi” katika hafla iliyofanyika baada ya mazungumzo yao. Erdogan alisema ameheshimiwa kuwa mtu wa kwanza kupokea tuzo hiyo, akiitaja kama ishara ya kuthaminiwa kwa kiwango cha juu kwa Uturuki na wananchi wake, na akamshukuru Tokayev kwa kuimarisha uhusiano wa mataifa hayo mawili.

Viongozi hao wawili pia walizindua Shule ya Msingi ya Khoja Ahmed Yasawi, iliyojengwa na nchi ya Kazakhstan katika wilaya ya Nurdagi, mkoa wa Gaziantep nchini Uturuki, kufuatia matetemeko makubwa ya ardhi ya Februari 6, 2023.

CHANZO:AA