| Swahili
UTURUKI
1 dk kusoma
Erdogan na Lula wajadili kuimarisha zaidi uhusiano wa kiuchumi katika mazungumzo ya simu
Rais wa Uturuki, Recep Tayyip Erdogan, amesema kuwa ushirikiano mpana zaidi katika uwekezaji, biashara na sekta ya viwanda vya ulinzi utanufaisha nchi zote mbili.
Erdogan na Lula wajadili kuimarisha zaidi uhusiano wa kiuchumi katika mazungumzo ya simu
Rais wa Uturuki Erdogan na Rais wa Brazil Lula da Silva wamejadili uhusiano wa mataifa mawili na sera zinazolenga amani kuhusu masuala ya kikanda. / / TRT World and Agencies

Rais wa Uturuki, Recep Tayyip Erdogan, na mwenzake wa Brazil, Luiz Inacio Lula da Silva, wamejadili uhusiano kati ya nchi zao pamoja na masuala ya kikanda na ya kimataifa, kwa mujibu waa Kurugenzi ya Mawasiliano ya Uturuki.

Katika mazungumzo hayo ya simu yaliyofanyika Jumatatu, Erdogan alipongeza kuimarika kwa uhusiano kati ya Uturuki na Brazil. Amesema uhusiano huo una msingi imara uliowekwa miaka 20 iliyopita.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Erdogan amesema kuwa kuimarisha ushirikiano katika maeneo yote, hasa uwekezaji, biashara na sekta ya viwanda vya ulinzi, kutakuwa na manufaa kwa nchi zote mbili.

Pia alisema anaamini kuwa Uturuki na Brazil zinaweza kuanzisha mfumo wa ushirikiano wa kiuchumi ambao utaongeza ustawi wa wananchi wa nchi zote mbili, hasa wakati ambapo kuna mwelekeo wa baadhi ya nchi kufuata sera za kulinda masoko yao ya ndani.

Aidha, Erdogan amesema kuwa sera zinazolenga amani ambazo Uturuki na Brazil zinafuata kuhusu masuala ya kikanda na kimataifa zinachangia katika amani ya dunia.

CHANZO:AA