Uingereza kusitisha viza za wanafunzi kutoka Cameroon, Sudan
Wizara ya Mambo ya Ndani inasema idadi ya wanafunzi wanaoomba hifadhi ya kisiasa kutoka nchi zilizoathirika "imeongezeka sana."
Serikali ya Uingereza imetangaza kuwa itasitisha kutoka viza za masomo kwa wanafunzi kutoka mataifa ya Cameroon na Sudan, pamoja na Afghanistan na Myanmar, ikiwa ni sehemu ya kukabiliana na wanaoomba hifadhi.
Wizara ya Mambo ya Ndani ilisema siku ya Jumanne kuwa idadi ya wanafunzi wanaoomba hifadhi kutoka mataifa hayo imeongezeka zaidi, na karibu maombi 135,000 ya watu waliingia Uingereza kwa njia hali tangu 2021.
"Daima Uingereza itaendelea kuwapa hifadhi watu wanaokimbia vita na mateso, lakini mifumo yenu ya viza yasitumiwe vibaya," anasema Waziri wa Mambo ya Ndani Shabana Mahmood katika taarifa. "Ndiyo maana nachukuwa hatua madhubuti kukataa viza kwa raia kutoka mataifa hayo wanaotaka kutumia vibaya ukarimu wetu."
Wizara ya Mambo ya Ndani inasema idadi ya wanafunzi wanaoomba hifadhi kutoka nchi za Afghanistan, Cameroon, Myanmar, na Sudan "imeongezeka" kwa zaidi ya asilimia 470% kati ya 2021 na 2025.
Mashua za wahamiaji
Uhamiaji umekuwa suala kubwa katika siasa za Uingereza, huku chama cha mrengo wa kulia cha Reform UK ikikipata umaarufu zaidi katika kura za maoni kwa msimamo wake wa kupinga uhamiaji.
Serikali kadhaa zimeshindwa kukabiliana na tatizo la mashua zinazopitia mkondo wa Ufaransa, ambazo huwa na idadi kubwa ya wahamiaji wasio na hati za kusafiri. Lakini mamlaka pia zinakabiliwa na shinikizo la kupunguza idadi ya wanaoomba ambao wanapitia kutumia njia zingine.
Wizara ya Mambo ya Ndani inasema serikali "imepunguza maombi ya wanafunzi kwa asilimia 20% katika kipindi cha mwaka 2025; hatua zaidi zinahitajika kutokana na wale wanaoingia kwa vzia za wanafunzi watakuwa asilimia 13% ya sehemu ya wale wanaoomba hifadhi".