Umoja wa Afrika waitaka Israel kubatilisha utambuzi wa Somaliland

Baraza la Masuala ya Kisiasa, Amani na Usalama la Umoja wa Afrika (AU) lilitoa wito Jumanne kwa Israel kubatilisha mara moja utambuzi wa Somaliland.

By
Umoja wa Afrika (AU) umeilaani Israel kwa kuitambua Somaliland kama taifa huru. / / Reuters

Waziri wa Mambo ya Nje wa Israel, Gideon Sa’ar, alitembelea Somaliland siku ya Jumanne katika ziara iliyoplaaniwa vikali na Somalia, siku 10 baada ya Israel kuitambua rasmi eneo hilo lililojitangaza kuwa taifa huru.

“Baraza la (AU) linalaani vikali, hatua ya upande mmoja ya Israel ya kuitambua eneo lililojitangaza kama ‘Jamhuri ya Somaliland’,” baraza hilo ilisema hilo kupitia mtandao wa X baada ya kikao cha mawaziri.