| Swahili
ULIMWENGU
2 dk kusoma
Benki ya Dunia na Qatar kusaidia kusambaza umeme kwa watu milioni 300 barani Afrika
Makubaliano kati ya Benki ya Dunia na Qatar pia yanajumuisha kutengenezwa kwa ajira na kusaidia nchi zilizoathiriwa na migogoro ya silaha.
Benki ya Dunia na Qatar kusaidia kusambaza umeme kwa watu milioni 300 barani Afrika
Mkataba kati ya Benki ya Dunia na Qatar ulitiwa saini siku ya Jumapili Januari 25. / Wengine / Others

Benki ya Dunia (WBG) na Mfuko wa Maendeleo wa Qatar (QFFD) wamesaini Hati ya Makubaliano (MoU) ili kuimarisha ushirikiano wa kimkakati katika kutoa suluhisho bunifu na endelevu za maendeleo duniani kote, ikiwemo kuongeza upatikanaji wa huduma za umeme katika nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara.

Makubaliano hayo, yaliyosainiwa wakati wa ufunguzi rasmi wa ofisi ya Benki ya Dunia mjini Doha siku ya Jumapili, yanatarajiwa kusaidia utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Qatar 2030 na kuimarisha ushiriki wa Benki ya Dunia na sekta za umma na binafsi za Qatar.

Ofisi hiyo pia itatumika kama jukwaa la kukuza uwekezaji wa nje kuelekea masoko yanayoibuka katika eneo hilo na duniani kwa ujumla.

Ushirikiano huu unaakisi dhamira ya pamoja ya kuendeleza ufadhili bunifu wa maendeleo, kusaidia ujenzi upya, kuimarisha uchumi, na kutengeneza ajira katika Mashariki ya Kati, Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara, pamoja na maeneo yaliyoathiriwa na migogoro.

Kupitia uhamasishaji wa zana za sekta ya umma na binafsi, ushirikiano huu utalenga kufungua fursa katika sekta muhimu, uthabiti, na ukuaji jumuishi, ikiwemo maendeleo ya rasilimali watu, nishati na madini, biashara ya kilimo, na maendeleo ya kidijitali.

Kuimarisha fursa za kiuchumi

Katika makubaliano ya WBG na QFFD wanakusudia kushirikiana katika kusaidia nchi zinazostahiki kupewa vipaumbele vya maendeleo ya kimataifa. Hii inajumuisha juhudi za kupanua upatikanaji wa umeme kwa watu milioni 300 katika Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara kupitia mpango wa M-300, na kuboresha maisha ya wakulima wadogo milioni 250 duniani kupitia jukwaa la AgriConnect la Benki ya Dunia.

Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Fahad Hamad Al-Sulaiti, Mkurugenzi Mkuu wa QFFD, alisema: “Hatua hii muhimu inaakisi dhamira ya muda mrefu ya Taifa la Qatar ya kuimarisha ushirikiano na taasisi kuu za kimataifa za kifedha na kuharakisha utekelezaji wa programu za maendeleo endelevu, kulingana na malengo ya Dira ya Taifa ya Qatar 2030.”

Rais wa Benki ya Dunia, Bw. Ajay Banga, alisema: “Ushirikiano wetu na Mfuko wa Maendeleo wa Qatar unaoanisha vipaumbele vya kimkakati vya pamoja na uwezo wa kukakamilishana ili kuimarisha kutengenezwa kwa ajira—na kuimarisha fursa za kiuchumi katika maeneo ambako ajira ni muhimu kwa uthabiti wa muda mrefu.”

Hatua hii pia inaendelea kuimarisha nafasi ya Qatar kama kitovu cha kimataifa cha ushirikiano wa kiuchumi na kifedha, na inaangazia jukumu la QFFD kama kichocheo cha ushirikiano wa kimataifa wenye athari chanya katika kuendeleza maendeleo ya haki na endelevu.

CHANZO:TRT Afrika
Soma zaidi
Maandamano Ufaransa yakigeuka kuwa ya vurugu, huku maelfu wakikamatwa katika miji tofauti
Maelfu ya Waisraeli waandamana Tel Aviv kudai kukomeshwa kwa enzi ya Netanyahu kabla uchaguzi
Papa Leo XIV ahairisha ziara ya Assisi kwa ushauri wa madaktari
Marekani yawaagiza wanadiplomasia wake na familia zao kuondoka nchi za Ghuba
Trump asema Marekani haijadiliani na Iran, aashiria kuwashughulikia 'hivi karibuni'
Iran kuzindua bomu lake kubwa zaidi “father of all bombs”
Uturuki, Qatar, Indonesia na Pakistan zasaini makubaliano ya ushirikiano wa ulinzi ya 'Badr'
Uingereza kupeleka ndege za kivita Saudi Arabia kuilinda dhidi ya mashambulizi ya Wahouthi
Makamu wa Rais wa Ufilipino, Sara Duterte apinga kung’olewa madarakani
Dereva amgonga mbunge wa Australia, amwacha mahututi
Waziri wa Ulinzi wa Marekani Pete Hegseth akutana na Netanyahu katika ziara ya kushtukiza Israel
Shambulio la Wahouthi lauwa watu kadhaa katika kituo cha mafunzo ya kijeshi Yemen
Machafuko ya Ulaya yafichua madhila ya uchumi, ufisadi na mzigo wa madeni
Mahakama Marekani yatoa hati ya kukamatwa kwa kiongozi wa zamani wa Cuba Raul Castro
Maandamano nchini Albania yaingia siku ya sita huku Waziri Mkuu Rama akikataa wito wa kujiuzulu
Wahouthi washambulia Ikulu ya Yemen kwa makombora, 5 wauawa
Saudi Arabia yazuia kombora katika anga ya mji wa Madinah
Urusi yaituhumu Ukraine kwa kushambulia mitambo yake ya kusafishia mafuta
Ujerumani yapiga marufuku matumizi ya pombe kwenye vituo vya treni
Marekani kutumia bomu lake kubwa zaidi dhidi ya Iran