| Swahili
AFRIKA
1 dk kusoma
Jeshi la Burkina Faso 'lawakata makali' magaidi zaidi 400 katika mashambulizi
Jeshi linasema kuwa limefanya mashambulizi hayo baada ya kambi yao kushambuliwa.
Jeshi la Burkina Faso 'lawakata makali' magaidi zaidi 400 katika mashambulizi
PICHA YA MAKTABA: Wanajeshi wa Burkina Faso wakishika doria katika barabara ya Gorgadji eneo la Sahel, Burkina Faso / Reuters

Jeshi la Burkina Faso linasema limekabiliana na mashambulizi ya makundi yenye silaha katika kambi mbalimbali za kijeshi Juni 30, na kuwaua watu zaidi ya 400 wakisaidiwa na mashambulizi ya angani.

Katika taarifa iliyotolewa Jumatano usiku, Uongozi wa Jeshi umesema kambi zimeshambuliwa katika maeneo ya Gayeri, Sirba, Solhan na Sebba, Kanda ya Liptako Region.

Kulingana na jeshi, vikosi vya ardhini, pamoja na vingine, vilikabiliana na mashambulizi hayo.

Jeshi linasema lilifanya mashambulizi ya angani na ardhini na kufanikiwa "kuwakata makali magaidi zaidi ya 400” na kupata pikipiki zaidi ya 250, silaha 353 na vifaa vingine vya mawasiliano.

Wanajeshi waliuawa

Jeshi pia liliripoti kuwa wanajeshi watatu waliuawa wakati wa mapigano hayo, ikiwemo wawili Solhan na mmoja Gayeri.

“Operesehani ya kuhakikisha usalama eneo hilo inaendelea na tunawasaka wale waliokimbia na kuhakikisha usalama wa raia,” jeshi lilisema, likitoa wito kwa raia kushirikiana na vikosi vya usalama, kufuata masharti ya usalama, na kutoa taarifa kuhusu mtu yeyote wanaemtilia shaka.

Taarifa hiyo ya mashambulizi ilihusisha Burkina Faso kuvunja uhusiano wa kidiplomasia na Ufaransa. Inadai Ufaransa inaunga mkono makundi yenye silaha,madai ambayo Ufaransa inakanusha.

Ufaransa inasema inatafakari kuhusu hatua watakayochukua baada ya Burkina Faso kuvunja uhusiano wa kidiplomasia.

CHANZO:TRT Afrika and agencies