Wagombea Urais Uganda 2026
Rais Yoweri Museveni ambae amekuwa madarakani tangu 1986 ni miongoni mwa wagombea wanaotaka kuchaguliwa kwa awamu nyengine.
Uganda itakuwa na Uchaguzi Mkuu Januari 15, 2026.Kuna jumla ya wagombea 8 wanaowania nafasi ya urais wa nchi hiyo.
Rais Yoweri Museveni ambae amekuwa madarakani tangu 1986 ni miongoni mwa wagombea wanaotaka kuchaguliwa kwa awamu nyengine.
Ahadi yake kwa wananchi Uganda ni kuifanya nchi hiyo kuwa ya kipato cha kati kwa kukuza viwanda, kuongeza thamani ya mauzo ya nje ya kilimo kama vile kahawa na pamba na kufaidika na kuanza kwa uzalishaji wa mafuta unaotarajiwa baadaye mwaka huu.
Msanii maarufu Robert Kyagulanyi mwenye umri wa miaka 43 anaonekana kuwa mpinzani mkuu wa Museveni akipeperusha bendera ya chama cha Nataional Unity platform(NUP).
Akifahamika kwa jina la ‘Bobi Wine’ na pia "rais wa gheto" wakati mmoja, anaonekana kujumuisha matarajio ya vijana ya mabadiliko na pia ameapa kukomesha ufisadi, kuimarisha ajira kwa vijana na kupitia upya mikataba na makampuni ya kimataifa ya mafuta ikiwa hayapendelei maslahi ya Waganda.
Hili ni jaribio lake la pili katika nafasi ya juu baada ya kushiriki katika kura za 2021.
Robert Kasibante mwenye umri wa miaka 38 mgombea chini ya Chama cha National Peasants Party( NPP) alijulikana kwa muda mrefu kwa kuendesha shule ya urembo huko jijini Kampala.
Sasa ndiye mgombea wa chama hicho kilichoanzishwa mwaka 2004. Mpango wake ni kukuza sekta ya kilimo ambayo inategemewa zaidi na wakulima wadogo ili kuwawezesha kupata manufaa zaidi.
Frank Bulira Kabinga ndiye mgombea urais wa Chama cha Revolutionary People's Party (RPP) katika uchaguzi mkuu wa 2026.
Alikuwa mwalimu wa shule ya upili, Bulira ni mtetezi mkubwa wa siasa za ushirikisho na mageuzi mengine ya utawala.Joseph Mabirizi ana taaluma ya Uinjilisti na anajulikana kwa kuanzisha makanisa katika sehemu za nchi.
Chama chake ni Conservative Party ( CP).Alishiriki katika uchaguzi wa urais mwaka 2016 na akapata kura chache zaidi. Anasema akichaguliwa mara hii atawaachilia wafungwa wote wa kisiasa ndani ya siku 100.
Nandala Mafabi ni mhasibu, mwanasheria, mchumi, na mwanasiasa mkongwe wa upinzani akiwa mmoja wa watu anaosifiwa kuwa na uzoefu mkubwa katika siasa za vyama vingi vya Uganda.Mafabi anagombea kupitia chama cha Forum for Democratic Change ( FDC).
Anasema matatizo ya Uganda yamejikita katika ufisadi, umaskini na ukosefu wa haki. Akisisitiza kuwa wakati amani inatawala nchini kinachohitajika sasa ni ajira na umiliki wa ndani.
Gregory Mugisha Muntu ni mwanasiasa wa Uganda na afisa mstaafu wa kijeshi. Yeye ndiye rais wa sasa wa chama cha Alliance for National Transformation (ANT) chama cha kisiasa alichokianzisha mwaka wa 2019.
/
Aliwahi kuwa Kamanda wa Jeshi, nafasi ya juu zaidi katika jeshi la Uganda, kutoka 1989 hadi 1998.Hili ni jaribio lake la pili katika nafasi ya juu kuwania nafasi hiyo mnamo 2021.
Anaahidi mabadiliko makubwa ya kisiasa ambayo yatawaweka wananchi katikati.Mubarak Munyagwa ni rais wa chama cha Common Man.
Ameahidi kutoa haki katika mgawanyo wa rasilimali.
Pia amesema atapiga marufuku Kiswahili kama lugha ya taifa nchini Uganda iwapo atachaguliwa kuwa rais.
Wananchi zaidi ya milioni 21 waliojisajili kupiga kura wataamua ni nani wanamtaka awe rais wao ifikapo Januari 15.