tokea masaa 8
Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa amekutana na Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Leo wa 14, siku ya Ijumaa, mazungumzo yakijikita kwenye hali ya usalama katika eneo la Mashariki ya Kati.
Macron alifika Vatican Ijumaa asubuhi, ambapo pia anatarajiwa kukutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Vatican, Kardinali Pietro Parolin.
Kulingana na Macron, mazungumzo hayo yamegusia namna ya kutafuta suluhu kuhusiana na mgogoro katika eneo la Mashariki ya Kati.
Kikao hicho kinakuwa cha kwanza kati ya wawili hao tangu Papa Leo achaguliwa kuliongoza Kanisa Katoliki duniani, mwaka 2025.
CHANZO:AA








