| Swahili
UTURUKI
2 dk kusoma
Uturuki yaonya dhidi ya uingiliaji wa nje nchini Iran, yatoa wito wa suluhu za ndani
Uturuki imeonya kuwa uingiliaji wowote wa nje katika nchi jirani ya Iran utaongeza na kuzidisha migogoro, si tu nchini humo bali pia katika eneo lote.
Uturuki yaonya dhidi ya uingiliaji wa nje nchini Iran, yatoa wito wa suluhu za ndani
"Hatutamani kamwe kuona machafuko yoyote kutokea katika nchi jirani ya Iran," Celik alisema. / / AA
12 Januari 2026

Uturuiki imesisitiza kuwa matatizo ya ndani ya Iran yanapaswa kutatuliwa kupitia mazungumzo na mienendo ya kijamii ya taifa hilo lenyewe.

Msemaji wa Chama cha AK na Naibu Mwenyekiti wake, Omer Celik, alisema siku ya Jumatatu kuwa Uturuki haitamani kuona machafuko yakitokea Iran, licha ya kukiri kuwa kuna changamoto ndani ya jamii ya Iran na taasisi zake za serikali.

“Hatutamani kamwe kuona machafuko yoyote yakizuka kwa jirani yetu Iran,” Celik alisema katika mkutano na waandishi wa habari katika makao makuu ya chama hicho mjini Ankara, baada ya kikao kilichoongozwa na Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan.

Alisema kuwa, kama alivyobainisha Rais wa Iran Masoud Pezeshkian, suluhu ya matatizo ya Iran inapaswa kupatikana kupitia suluhu za ndani za jamii ya Iran na dhamira ya kitaifa ya nchi hiyo.

Kuongezeka kwa machafuko

“Uingiliaji wa nje utasababisha madhara makubwa zaidi,” Celik alisema, akiongeza kuwa hasa uingiliaji unaochochewa na Israel unaweza kupelekea migogoro mikubwa na kuyumbisha zaidi utulivu wa eneo zima.

Akisisitiza kuwa suala hilo linapaswa kushughulikiwa kupitia mazungumzo, majadiliano na kuzidisha mawasiliano, Celik alisema kauli za hivi karibuni za maafisa wa Israel zinazolenga Iran zina hatari ya kuchochea mvutano mpana wa kikanda.

“Mtazamo huu wa uchokozi utasababisha misukosuko mikubwa zaidi katika eneo lote na unapaswa kukataliwa kabisa,” alisema.

Kwa sasa Iran inashuhudia wimbi lake kubwa zaidi la maandamano tangu mwaka 2022. Wakati huo huo, Rais wa Marekani Donald Trump amesema Washington inaweza kuingilia kati endapo nguvu zitatumika dhidi ya waandamanaji, jambo linaloongeza hofu ya kuongezeka kwa mvutano na mgogoro zaidi.

CHANZO:AA
Soma zaidi
Makamu wa Rais wa Uturuki akutana na balozi wa Brazil
Idadi ya watu nchini Uturuki yafikia milioni 86 kwa mwaka 2025
Uturuki yalaani shambulizi la RSF nchini Sudan
Matetemeko ya ardhi ya Uturuki 2023 yalisababisha hasara ya dola bilioni 250: Erdogan
Fidan wa Uturuki akutana na Kamishna wa Maswala ya Wanachama wa EU, kujadili masuala ya ushirikiano
Rais wa Uturuki aadhimisha kumbukumbu ya miaka 3 ya tetemeko la ardhi
Uturuki imelaani shambulizi la kigaidi nchini Nigeria lililoua takriban watu 170
Uturuki kuimarisha uwepo wake wa kijeshi kuisaidia Somalia kupambana na ugaidi
Uturuki na Saudi Arabia kuimarisha ushirikiano wa ulinzi na uwekezaji katika ndege za kivita za KAAN
Mke wa Rais wa Uturuki amekutana na mwenzake wa Misri jijini Cairo
Erdogan na Sisi waimarisha ushirikiano kati ya Uturuki na Misri wajadili Gaza na migogoro ya kikanda
Kikao cha mwisho cha Jukwaa la Biashara kati ya Uturuki na Misri chafunguliwa jijini Cairo
Erdogan na Mwanamfalme wa Saudia waunga mkono umoja wa Somalia, wajadili masuala ya kikanda
Rais wa Uturuki Erdogan akutana na Mwanamfalme wa Saudia Mohammed bin Salman jijini Riyadh
Uturuki yapongeza hatua zinazoimarisha amani, utulivu nchini Syria: Erdogan
Uturuki yasema kuongeza mamlaka ya ujumbe wa amani wa UN bila kushirikisha Kupro ya Uturuki ni kosa
Televisheni ya kitaifa ya Uturuki TRT yaadhimisha miaka 58 ya utangazaji
Iran iko 'tayari' kwa 'makubaliano ya nyuklia ya haki na ya usawa': mwanadiplomasia mkuu
Uturuki iko tayari kusuluhisha mvutano kati ya Marekani na Iran: Erdogan amwambia Pezeshkian
Uturuki inakuwa moja ya kituo chenye ushawishi wa kisiasa duniani: rais wa Uzbekistan