| Swahili
MICHEZO
1 dk kusoma
Jela ‘yanukia’ kwa kocha wa Real Madrid Carlo Ancelotti
Kocha huyo, ambaye ameipa Real Madrid mataji matano la Ligi ya Mabingwa Ulaya (UEFA), anakabiliwa na shitaka la kushindwa kulipa Dola Milioni 1.1 wakati wa msimu wake wa kwanza nchini Hispania.
00:00
Jela ‘yanukia’ kwa kocha wa Real Madrid Carlo Ancelotti
Akiwa kizimbani siku ya Jumatano, Ancelloti alikana kutenda kosa hilo kwa makusudi./Picha: Getty / Getty Images

Kesi ya ukwepaji kodi iliyokuwa ikimkabili Kocha wa Real Madrid Carlo Ancelotti imemalizika siku ya Alhamisi, huku waendesha mashitaka wa nchini Hispania wakitaka mtaliano huyo apewe hukumu ya miaka minne na miezi tisa.

Kocha huyo, ambaye ameipa Real Madrid mataji matatu ya la Ligi ya Mabingwa Ulaya (UEFA), anakabiliwa na shitaka la kushindwa kulipa Dola Milioni 1.1 wakati wa msimu wake wa kwanza nchini Hispania.

Kulingana na waendesha mashitaka wa nchini Hispania, kocha huyo mwenye umri wa miaka 65, alijitengenezea mfumo wa kuficha malimbikizo yake ya mapato kupitia biashara ya nyumba, huku akiwasilisha taarifa za mishahara yake pekee.

"Huu ni ulaghai," alisema kiongozi mmoja wa mashitaka jijini Madrid, akiongeza kuwa ilikuwa ni vigumu kuamini kauli ya Ancelotti kuwa “hakuwa anaelewa alichokuwa anakifanya.”

Kulingana na mfumo wa sheria wa Hispania, waendesha mashitaka wanaweza kuongeza mashitaka au hata kumuondolea mtu kesi na kubadilisha aina ya hukumu, kutegemeana na ushahidi uliowasilishwa.

Akiwa kizimbani siku ya Jumatano, Ancelloti alikana kutenda kosa hilo kwa makusudi.

Kocha huyo aliiambia mahakama kuwa alipata ushauri wa waajiri wake, kabla kutenda kosa hilo.

CHANZO:AFP