Netanyahu asema Israel itaishambulia Hezbollah pale inapobidi
Wakati huo huo, jeshi la Israel limesema kuwa linaendelea na operesheni za nchi kavu kusini mwa Lebanon, ambako vikosi vya Israel vinapambana na Hezbollah toka mwezi wa tatu.
Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu amesema nchi yake kikundi cha Hezbollah, chenye kuungwa mkono na Iran pale inapobidi.
"Tunaendelea kuishambulia Hezbollah kwa nguvu zote," alisema Netanyahu kupitia ukurasa wake wa X.
"Ujumbe wetu uko wazi, yeyote anayekwenda kinyume na raia wa Israel, tumshambulia tu. Tutaendelea kuipiga pale inapobidi hadi pale usalama wa wakazi wa magharibi ya Israel utakaporejea,” aliongeza.
Wakati huo huo, jeshi la Israel limesema kuwa linaendelea na operesheni za nchi kavu kusini mwa Lebanon, ambako vikosi vya Israel vinapambana na Hezbollah toka mwezi wa tatu.
Katika hatua nyingine, Israel imesema kuwa imeshambulia vivuko viwili muhimu vinavyotumiwa na magaidi wa Hezbollah kutoka kaskazini kuelekea kusini mwa Mto Litani nchini Lebanon.
Kivuko hicho hutumika kusaifiri silaha nzito za kijeshi.