Aliou Cisse achukua mikoba ya kuifundisha Angola baada ya kuachana na Libya

Mchezaji huyo wa zamani mwenye umri wa miaka 50, amesaini mkataba wa miaka minne na Angola, akitarajiwa kuisaidia Angola kufuzu fainali za Kombe la Dunia mwaka 2030, baada ya kushindwa kufanya hivyo mwaka huu.

By
Kocha Aliou Cisse./Picha:Wengine

Shirikisho la sola la Angola (FAF) limemtangaza Aliou Cisse kama kocha mpya wa timu ya taifa ya nchi hiyo.

Cisse anachukua mikoba ya kuifundisha Angola, saa 24 baada ya kujiuzulu kuifundisha timu ya taifa ya Libya.

Cisse, ambaye aliiongoza Senegal kutwaa kombe la AFCON  mwaka 2022, aliachana na timu ya taifa ya Libya, ikiwa ni miezi kumi tangu achukue mikoba hiyo, Machi 2025.

Mchezaji huyo wa zamani mwenye umri wa miaka 50, amesaini mkataba wa miaka minne na Angola, akitarajiwa kuisaidia Angola kufuzu fainali za Kombe la Dunia mwaka 2030, baada ya kushindwa kufanya hivyo mwaka huu.

"Leo ni siku ya kipekee kwetu, siku ya matumaini na maono kwa mustakabali wa soka letu,” alisema rais wa FAF, Alves Simoes, wakati wa hafla ya kumtambulisha kocha huyo mpya jijini Luanda.