Mkuu wa Shirika la Ujasusi wa Uturuki Ibrahim Kalin amekutana na Mwenyekiti wa Kitengo cha Siasa cha Hamas Khalil al-Hayya na ujumbe wake jijini Istanbul, ambapo walijadili juhudi za kuendeleza mchakato wa hatua ya pili ya mpango wa amani wa Gaza, kulingana na vyanzo.
Mkutano huo uliangazia mchakato ulioandaliwa kwa ajili ya kuelekea hatua ya pili ya mpango wa amani, huku washiriki wakisisitiza kuhusu ari ya Hamas kuhusu pendekezo hilo, vyanzo hivyo viliiambia Anadolu agency.
Pande zote mbili zimeeleza wasiwasi kuwa Israel imeendeleza mashambulizi ya kijeshi Gaza badala ya kuangazia mchakato huo.
Walisisitiza kuwa jamii ya kimataifa inatakiwa kuchukua hatua ili kuzuia mashambulizi ya Israel mara moja.
Kuhamasisha jamii ya kimataifa
Washiriki pia walijadili kuhusu ukiukwaji wa haki za Wapalestina katika eneo linalokaliwa la Ukingo wa Magharibi na Jerusalem Mashariki huku mauaji ya halaiki ya jeshi la Israel yakiendelea Gaza.
Walieleza kuhusu ulowezi wa Israel unaoendelea katika maeneo yanayokaliwa na kuongezeka kwa vurugu kutoka kwa walowezi wa Israel.
Hali kwa watu wa Gaza pia ilijadiliwa wakati wa mkutano huo, na Uturuki ikasisitiza msimamo wake wa kuunga mkono Gaza kwa juhudi za kisiasa na mipango yenye lengo la kuimarisha utoaji misaada kwa watu, vyanzo vilisema.
Mkutano huo pia ulisisitiza kuhusu juhudi za Uturuki kuhamasisha jamii ya kimataifa katika kumaliza ukatili wa Israel Gaza, kuzuia ukiukwaji wa hali za Wapalestina katika maeneo yanayokaliwa ya Ukingo wa Magharibi na Jerusalem Mashariki, pamoja na kuongeza misaada kwa watu katika eneo hilo.
Washiriki walieleza kuhusu juhudi za pamoja za Uturuki, Qatar na Misri katika kusaidia kupatikana kwa amani Gaza.
Ujumbe wa Hamas pia ulimshkuru Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan kwa juhudi za Uturuki katika kusaidia kupatikana kwa amani Gaza.




















