| Swahili
Maoni
ULIMWENGU
4 dk kusoma
Je, China inaweza kubadilisha uhusiano wao na Iran kuwa wa kidplomasia kabla ya mkutano wa Xi-Trump?
Huku wito ukiendelea kutolewa kwa Iran na Marekani kurudi katika majadiliano, mazungumzo ya Araghchi nchini China baada ya kufahamu Xi Jinping anataka nini wakati atakapokutana na Donald Trump.
Je, China inaweza kubadilisha uhusiano wao na Iran kuwa wa kidplomasia kabla ya mkutano wa Xi-Trump?
Vita vya Iran vinatarajiwa kuwa miongoni mwa masuala yatakayojadiliwa wakati Xi na Trump watakapokutana.

Na Zeynep Conkar

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Abbas Araghchi amekutana na mwenzake wa China Wang Yi jijini Beijing mapema wiki hii, huku Iran ikitazamia mmoja wa washirika wake wa kimataifa kuwaunga mkono huku vita vya Marekani na Israel dhidi ya Iran vikiendelea.

Mazungumzo hayo yanajiri baada ya Rais wa China Xi Jinping kutoa wito kwa mataifa ya BRICS kusaidia katika upatanishi wa kumaliza vita ikiwa ni zaidi ya wiki moja kabla ya Xi kukutana na Rais wa Marekani Donald Trump jijini Washington Septemba 24.

Muda wa mkutano huu umefanya China kuangaziwa: China imekuwa ikitoa wito wa kutumika kwa diplomasia na kumaliza vita, huku wakiendeleza ushirikiano wa kisiasa na kiuchumi na Iran. 

Uhusiano wa karibu wa China na Iran, pamoja na uchumi wake mzuri, unaweza kuwapa China ari ya kumaliza mapigano kabla ya mkutano wa Xi na Trump, kulingana na Profesa Garth Le Pere, mchambuzi wa masuala ya kimataifa na pia Profesa wa muda katika Chuo Kikuu cha Pretoria.

“Kulingana na muungano wa karibu kati ya Iran na China, kuna matarajio kuwa China itatumia ziara ya Rais Xi jijini Washington kujaribu kusitisha mapigano na kutuliza uhasama,” Le Pere aliiambia TRT World.

“China inajiona kama isiyoegemea upande wowote na inajaribu kuwa mpatanishi anayeaminiwa, pamoja na kuwa hilo haliko wazi,” aliongeza.

Wakati wa mkutano na Araghchi, Wang alitoa wito kwa Iran na Marekani kutuliza hali, kurudi katika makubaliano yaliyofikiwa katika majadiliano ya Islamabad kufikia sasa. 

Pia alitoa wito kwa mashauriano zaidi kati ya pande zote mbili na kutaka hatua zichukuliwe za kufunguliwa kwa Mlango Bahari wa Hormuz.

 Wakati huo huo, kuendelea kwa vita kunatishia usambazaji wa nishati, njia za biashara na uthabiti wa uchumi ambayo China inategemea.

Mlango Bahari wa Hormuz ni muhimu zaidi. 

Wang anatoa wito wa kufunguliwa kwake huku vita vikiendelea kutatiza njia muhimu ya nishati duniani. Viongozi wa BRICS pia wanatoa wito kwa kusitishwa kabisa mapigano na kuimarisha biashara duniani na kuruhusu nishati kusambazwa kwa kuzingatia azimio la New Delhi.

Nini mchango wa China katika mkutano wa Xi-Trump?

Mara ya mwisho kwa Wang kuwa mwenyeji wa Araghchi jijini Beijing ilikuwa mwezi Mei, kabla ya mkutano wa Rais wa Marekani Donald Trump na Xi katika mji mkuu wa China.

Mkutano wa Jumatano ulikuwa wa pili wa moja kwa moja katika mji mkuu wa China tangu Marekani na Israel walipoanzisha mashambulizi dhidi ya Iran Februari 28.

Kwa Iran, mkutano huo ni fursa ya kuweka wazi msimamo wake kwa China kabla ya Xi kuwa na kikao na Trump. Kwa China, ni nafasi ya kuisikiliza Iran kabla ya kuanza kikao na Marekani.

Vita vya Marekani na Israel dhidi ya Iran vinatarajiwa kuwa katika agenda wakati Xi na Trump watakapokutana, pamoja na masuala ya biashara, Taiwan na masuala mengine yanayoleta uhasama kati ya nchi hizo mbili.

“Mpango wa nyuklia wa Iran unatarajiwa kuwa muhimu zaidi kwa mazungumzo kati ya Araghchi na Wang, hasa tangu Marekani, Ufaransa, Ujerumani, na Uingereza kutaka shirika la IAEA hivi majuzi kuifikisha Iran kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa,” Le Pere anasema.

“Hata hivyo, hii zaidi kwa ishara tu. Jaribio lolote la kufanya maamuzi ya kuongeza vikwazo vya kwa Iran ambayo tayari inapitia matatizo huenda yakafeli kwa sababu China na Urusi watapiga kura ya turufu,” Le Pere anasema.

“Hata hivyo, China imehisi matatizo ya vikwazo vya Marekani dhidi ya Iran.”

China ina maslahi mengi ya kuweka sawa, kulingana na wataalamu. Inataka kuendeleza uhusiano wa kimkakati na Iran, kulinda ufikiaji wake wa nishati ya Iran na kupinga shinikizo ambalo litaonekana kudumaza maslahi yake. 

Wakati huo huo, kuna maslahi ya kuhakikisha vita haviendelei zaidi na kuzuia Iran isije ikawa chanzo kingine cha ukosefu wa uthabiti kwa uchumi duniani.

Hilo linawapa China uwezo, lakini uwezo siyo sawa na upatanishi.

Kwa sasa, China inaonekana kutumia nafasi yake kutaka pande zote mbili kuhusika katika diplomasia huku ikitoa nafasi ya kutumia njia zingine. 

CHANZO:TRT World