Bassirou Diomaye Faye: Rais wa Senegal
Basirou Diomaye Faye ni rais wa taifa la Senegal lililoko Afrika Magharibi. Taifa hilo lina watu takriban watu milioni 19.
Jina kamili la kiongozi wa taifa hilo ni Basirou Diomaye Diakhar Faye mzaliwa wa Ndiaganiao katika mji wa M’bour miaka 45 iliopita.
Ukiskia majina yanaumba maana yake ni hii kwa lugha ya Serer inayozungumzwa na baadhi ya watu wa Senegal na Gambia, jina ‘’Diomaye’’ maana yake ‘’Mheshimiwa’’ sasa limetimia au vipi?
Amekuwa rais wa nchi hiyo tangu mwaka April 2024. Yeye na Waziri Mkuu wake Ousmane Sonko walikutana wakiwa maafisa forodha.
Mwaka 2014 urafiki wao ukaimarika zaidi, Sonko alipounda chama cha kisiasa cha PASTEF.
Diomaye Faye alimsaidia sana Sonko katika uchaguzi wa urais wa 2019, lakini Sonko alimaliza wa tatu na asilimia 16 ya kura.
Kufa kufaana, mwaka 2021 Faye akawa Katibu Mkuu wa chama cha PASTEF baada ya Sonko kukamatwa.
Mwaka 2022 alijaribu kuunganisha upinzani na kufanikiwa kushinda viti 56 katika bunge la wajumbe 165. Alijaribu kutafuta umeya wa eneo la Ndianganao, lakini hakufanikiwa.
Alikamatwa mwaka 2023 kwa madai kadhaa kusambaza taarifa taarifa za uwongo ikiwa sehemu ya madai mengi aliyoshtumiwa nayo.
Kutokana na wasiwasi kuhusu mgombea wa urais wa chama cha PASTEF kwa kuwa Ousmane Sonko alikuwa yuko gerezani, chama hicho kilimchagua Faye licha ya yeye pia kuwa kizuizini.
Kwa kuwa chama cha PASTEF kilikuwa kimepigwa marufuku alikuwa agombee kama mgombea huru.
Aliachiliwa mwezi Machi, kabla ya hapo Sonko alitangaza kumuunga mkono. Kauli mbiu yake wakati wa kampeni za uchaguzi wa 2024 kwa lugha ya Wolof ilikuwa ‘’Diomaye mooy Sonko’’ maana yake ‘’Diomaye ni Sonko’’ kusisitiza ukaribu wao.
Alishinda uchagui huo wa mwezi Machi kwa asilimia 54 na kumfanya kuwa mgombea wa kwanza kushinda karika duru ya kwanza tangu nchi hiyo ya Senegal ilipopata uhuru wake kutoka kwa Ufaransa 1960.
Aliapishwa rasmi tarehe 2 Aprili kuwa rais na hatua ya kwanza aliyochukuwa ni kumteua Ousmane Sonko Waziri Mkuu ambaye aliwasilisha baraza lake la mawaziri siku tatu baadaye.
Rais Diomaye Faye ana wake wawili na amempa mtoto wake mmoja jina la rafiki yake Ousmane Sonko kwa heshima ya ukaribu wao.