| Swahili
AFRIKA
2 dk kusoma
UN yaelezea unyanyasaji wa kingono DRC, makundi yenye yatajwa kuhusika
Takriban asilimia 80% ya wale walioathirika wako katika mikoa ya mashariki ya Kivu Kaskazini na Kivu Kusini, data za Umoja wa Mataifa zinaonesha
UN yaelezea unyanyasaji wa kingono DRC, makundi yenye yatajwa kuhusika
DRC
tokea masaa 7

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (MONUSCO) siku ya Jumatatu imeonya kuhusu kuzidi kwa unyanyasaji wa kingono katika nchi hiyo yenye mgogoro, ukieleza kuwa makundi yenye silaha yanahusika kwa matukio mengi yaliyoorodheshwa 2025.

Ofisi ya Umoja ya Mataifa kuhusu Haki za Binadamu (UNJHRO) imeorodhesha matukio 887 yaliyohusisha waathiriwa 1,534, ikiwemo wanawake 854 na wasichana 672, kulingana na taarifa kutoka MONUSCO.

Mikoa ya mashariki ya Kivu Kaskazini na Kivu Kusini ndiyo yenye matukio mengi zaidi ikiwa na asilimia 80% ya waathiriwa, ilisema.

UNJHRO imebaini kuwa makundi yenye silaha yanahusika na kwa asilimia 75% ya waathiriwa, huku kundi la waasi la M23 likihusika na idadi kubwa ya matukio (439), likifuata na wapiganaji wa Wazalendo, CODECO, makundi mbalimbali ya Mai-Mai, FDLR, na ADF.

Pia ilieleza wasiwawasi kuhusu baadhi ya maafisa wa serikali, ikisema wanajeshi, polisi, na idara ya ujasusi imehusika karibu katika tukio moja kati ya matano ya unyanyasaji wa kingono.

UNJHRO imeonya kuwa ubakaji ulikuwa unatumiwa kama vita nchini Congo, huku wanawake na wasichana wakifanywa watumwa wa kingono na kizazi kingine cha watoto kikikumbwa na unyanyapaa na kutengwa.

Pia inaeleza kuhusu madhila ya watoto waliozaliwa kutokana na ubakaji, ambao hukataliwa na familia, kutosajiliwa, na wanakuwa katika hatari kubwa ya kutengwa kijamii na mara moja huchukuliwa na makundi yenye silaha.

MONUSCO inasema mbali na kuwa asilimia 70% ya walionusurika wanapata huduma za dharura za afya, ni chini ya asilimi 2% wanaopata usaidizi kamili, ikiwemo msaada wa kisheria, kisaikolojia, na wa kijamii.

CHANZO:AA