Waziri Mkuu wa Moldova Alexandru Munteanu amejiuzulu wadhifa wake, miezi nane baada ya kukaa madarakani.
Kupitia ujumbe wake aliouweka kwenye ukurasa wake wa Facebook siku ya Ijumaa, Munteanu alisema kuwa amefikia uamuzi huo baada ya "kusukumwa na misimamo yake na kile anachokiamini".
Hata hivyo, Rais wa Moldova, Mai Sandu amekana madai ya Munteanu, kuwa alikuwa akibanwa katika kutekeleza wajibu wake.
"Madai ya kuwa alidhibitiwa pale alipotaka kumbana na matumizi mabaya ya ofisi hayana ukweli wowote," alisema Sandu wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari.
"Alikuwa na uhuru na fursa ya kutekeleza wajibu wake ndani ya serikali."
Kwa sasa, Munteanu atabakia kuwa kiongozi wa mpito wa ndani ya serikali, wakati Sandu akijaribu kumpata mrithi wake.















