Idadi ya watu nchini Uturuki yafikia milioni 86 kwa mwaka 2025

Hii ni baada ya ongezeko la asilimia 5ya watu mwaka 2025, kutoka asilimia 3.4 mwaka 2024.

By
Kwa mujibu wa takwimu hizo, jiji la kibiashara la Istanbul, liliongoza likiwa na watu milioni 15.75, ambayo ni ongezeko la watu 52, 451./Picha:AA

Idadi ya watu nchini Uturuki imeongezeka na kufikia milioni 86.09, kwa mujibu wa takwimu rasmi za hivi karibuni.

Takwimu hizo zinaonesha kuwa idadi ya wanaume imefikia milioni 43.06 ambayo ni sawa na asilimia 50.02 ya watu wote, huku wanawake wakiwa ni milioni 43.03, sawa na asilimia 49.98, taasisi ya takwimu ya TurkStat ilisema siku ya Jumatatu.

“Uwiano wa watu waishio kwenye wilaya ilifikia asilimia 93.6 mwaka 2025, toka asilimia 93.4 mwaka 2024, huku ile wa mijini, ukishuka hadi asilimia 6.4 kutoka asilimia 6.6.”

Kwa mujibu wa takwimu hizo, jiji la kibiashara la Istanbul, liliongoza likiwa na watu milioni 15.75, ambayo ni ongezeko la watu 52, 451, ukilinganisha na mwaka jana.

Ilifuatiwa kwa karibu na mji mkuu wa Uturuki, Ankara ambao ulikuwa na watu milioni 5.9, Izmir ukiwa na watu milioni 4.5, Bursa (milioni 3.26), huku mji wa kitalii wa Antalya ukiwa na watu milioni 2.77.

Wastani wa umri wa watu nchini Uturuki umefikia 34.9 kwa mwaka 2025, kutoka 34.4 mwaka 2024.