Marekani na Venezuela zimeingia makubaliano, yatakayoiwezesha Marekani kuanza kuvuna dhahabu na mafuta kutoka taifa la Venezuela.
Makubaliano hayo, yalifikiwa siku ya Jumatano, pembezoni mwa mkutano wa G20, ulioandaliwa na Marekani.
Kampuni ya Kimarekani ya Continental Resources, iliyoasisiwa na Howard Hamm, ilisaini mkataba na shirika la mafuta la serikali ya Venezuela (PDVSA), wa kuendesha kitalu cha mafuta katika eneo la chanzo cha nishati hiyo, katika eneo la Orinoco.
Hamm, ambaye ni mshirika wa karibu wa Rais Donald Trump, alimbatana na maofisa wengine wa Venezuela wakati wa utiaji saini huo, ambao unajiri baada ya serikali ya Marekani kumuondoa madarakani Rais Nicolas Maduro, mwezi Januari mwaka huu.
Kwa upande wake, Waziri wa Nishati wa Marekani, Chris Wright ameelezea mkataba huo kama hatua muhimu katika kukuza uhusiano kati ya Marekani na Venezuela.






















