| Swahili
ULIMWENGU
2 dk kusoma
Shambulio jingine katika uwanja wa ndege wa Saudi Arabia; mmoja auawa na wengine 11 kujeruhiwa
Shambulio hilo linafuatia wimbi la mashambulizi yanayofanywa na kundi la Wahouthi katika viwanja vya ndege nchini Saudi Arabia. Mji wa Riyadh umelengwa mara mbili ndani ya saa 48. Shambulio la awali likiripotiwa kuua watu 13 na kujeruhi zaidi ya 300.
Shambulio jingine katika uwanja wa ndege wa Saudi Arabia; mmoja auawa na wengine 11 kujeruhiwa
Picha za kamera za usalama zinaonyesha shambulio katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa King Khalid nchini Saudi Arabia / / Reuters

Shambulio jingine la wapiganaji wa kundi la Wahouthi katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa King Khalid, katika mji mkuu wa Saudi Arabia, Riyadh, lasababisha kifo cha mtu mmoja na kuwajeruhi wengine 11.

Mamlaka ya Usafiri wa Anga ya Saudi Arabia (GACA) ilithibitisha mwishoni mwa juma kuwa mtu aliyefariki dunia alikuwa raia wa Pakistani anayeishi nchini humo. Aidha, watu 11 waliojeruhiwa walipelekwa hospitali kwa ajili ya matibabu.

Kwa mujibu wa mamlaka hiyo, shambulio hilo pia limesababisha uharibifu wa mali, ambao tathmini yake ilikuwa bado inaendelea.

Awali, muungano wa kijeshi unaoongozwa na Saudi Arabia nchini Yemen ulisema kuwa kifaa cha kurushwa kisichojulikana kilipiga Jengo la Abiria la Namba 4 katika uwanja huo wa ndege, Jumapili alasiri, na kusababisha moto.

Shambulio hilo limetokea siku moja tu baada ya shambulio jingine katika uwanja huo huo, ambalo kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa, liliua watu 12 na kujeruhi zaidi ya 300.

Mashambulizi yalenga sekta ya usafiri wa anga na miundombinu ya mafuta

Muungano wa kijeshi unaoongozwa na Saudi Arabia uliwalaumu wapiganaji wa kundi la Wahouthi kwa shambulio la awali na kuahidi kuchukua hatua kali za kukabiliana nao.

Muungano huo ulilitaja shambulio hilo kuwa ni ukiukaji wa sheria za kimataifa za kibinadamu.

Katika tukio jingine, Saudi Arabia ilitangaza kuwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa King Fahad, uliopo katika mji wa Dammam mashariki mwa nchi hiyo, nao pia umeshambuliwa.

Taarifa hiyo ilitolewa wakati wapiganaji wa kundi la Wahouthi nchini Yemen wakidai kutekeleza mashambulizi dhidi ya viwanja viwili vya ndege vya Saudi Arabia pamoja na miundombinu mikubwa ya mafuta.

Mamlaka ya Usafiri wa Anga ya Saudi Arabia (GACA) ilisema ilikuwa ikifanya tathmini ya uharibifu na ukaguzi wa usalama katika uwanja huo wa ndege, kwa kushirikiana na mamlaka husika.

Hata hivyo, mamlaka hiyo haikutoa maelezo zaidi kuhusu idadi ya vifo au majeruhi, wala kiwango cha uharibifu. Ilieleza kuwa tukio hilo limetokea wakati mashambulizi dhidi ya miundombinu ya usafiri wa anga ya kiraia nchini humo yakiendelea.

Wakati huohuo, muungano wa kijeshi unaoongozwa na Saudi Arabia ulitangaza kupitia mtandao wa X kuwa mifumo ya ulinzi wa anga ilinasa na kuangamiza ndege isiyo na rubani katika Mkoa wa Mashariki wa Saudi Arabia.

CHANZO:TRT World and Agencies
Soma zaidi
JD Vance anaongoza juhudi za kimya kimya kwa ajili ya makubaliano mapya ya Marekani na Iran
Hegseth anashikilia msimamo wake kuhusu vita dhidi ya Iran, huku Vance na Trump wakivilaumu
Rais wa Israel siku ya Jumapili kutangaza atakayeunda serikali mpya nchini humo
Nepal yaruhusu kilimo cha bangi
Panya buku mwenye kilogramu 30 agundulika Thailand
Kiongozi wa upinzani nchini Israel aondoa uwezekano wa kuunda serikali ya umoja na Netanyahu
Trump: Vita dhidi ya Iran vilichangia kushindwa kwa chama cha Republican katika uchaguzi
Wapiganaji wa Iran wadai kushambulia droni mbili za Marekani kwenye Mlango Bahari wa Hormuz
Ajali ya helikopta juu ya Mlima Everest yaua mtalii wa kihindi
Putin asema Urusi ni mshirika bora kwa Afrika kuliko nchi zenye historia ya ukoloni
Netanyahu aongoza, hatima ya kuunda serikali bado haijulikani
Rais Lula wa Brazil atimiza miaka 81, aahidi kufanya kazi saa 24
Lieberman ataka Netanyahu achunguzwe kwa tuhuma za uhaini kuhusiana na vita dhidi ya Iran
Rais wa Brazil Lula da Silva apata ushindi wa kihistoria wa muhula wa 4 dhidi ya Flavio Bolsonaro
Maandamano Ufaransa yakigeuka kuwa ya vurugu, huku maelfu wakikamatwa katika miji tofauti
Maelfu ya Waisraeli waandamana Tel Aviv kudai kukomeshwa kwa enzi ya Netanyahu kabla uchaguzi
Papa Leo XIV ahairisha ziara ya Assisi kwa ushauri wa madaktari
Marekani yawaagiza wanadiplomasia wake na familia zao kuondoka nchi za Ghuba
Trump asema Marekani haijadiliani na Iran, aashiria kuwashughulikia 'hivi karibuni'
Iran kuzindua bomu lake kubwa zaidi “father of all bombs”