| Swahili
MICHEZO
1 dk kusoma
Mabondia wa Uganda watoweka baada kumalizika kwa Michezo ya Jumuiya ya Madola Glasgow
Wanamasumbwi wanne kati ya sita wa Uganda wametoweka kabla ya kikosi hicho kurudi nyumbani Jumanne kama ilivyokuwa imeratibiwa, hii ni kulingana na taarifa za vyombo vya habari.
Mabondia wa Uganda watoweka baada kumalizika kwa Michezo ya Jumuiya ya Madola Glasgow
Hafla ya kufunga Michezo ya Jumuiya ya Madola mjini Glasgow.

Polisi wa Scotland wanachunguza taarifa za wanamichezo wa kigeni, wanaofahamika kuwa raia wa Uganda na Pakistan, ambao wameshindwa kurejea makwao baada ya kushiriki Michezo ya Jumuiya ya Madola mjini Glasgow Jumapili iliopita.

"Polisi wa Scotland wamepata taarifa za baadhi ya wanamichezo ambao hawajulikani waliko," msemaji alisema siku ya Jumanne.

"Uchunguzi unaendelea kwa sasa kutathmini mazingira waliotoweka, na pia tunawasiliana na Uhamiaji."

Shirika la habari la NBS Sport la Uganda liliripoti kuwa mabondia wanne kati ya sita wametoweka baada ya kutoonekana siku ya kusafiri kurudi nyumbani kama ilivyotarajiwa siku ya Jumanne na mmoja wao aliwaambia NBS Sport kuwa wanapanga kuomba hifadhi ya kisiasa.

Taarifa za kutoweka kwa wanamichezo baada ya Michezo ya Jumuiya ya Madola zimekuwa zikitokea katika makala ya michezo ya hivi karibuni, ambayo yamefanyika Australia au Uingereza tangu Glasgow 2014.

2018, baada ya Michezo ya Gold Coast nchini Australia, mamlaka zilikuwa bado zinawatafuta wanamichezo 50 na maafisa mwezi mmoja baada ya michezo hiyo kumalizika , na wengine 190 wakiomba hifadhi ya kisiasa.

Wanamichezo 3,000 kutoka nchi 74 walihudhuria Michezo hiyo ya Glasgow iliofanyika katika kipindi cha 11.

CHANZO:TRT Afrika Swahili