| Swahili
MICHEZO
1 dk kusoma
Vinicius Jr aizima ndoto ya Arsenal, asaini mkataba mpya na Real Madrid
Kabla ya kusaini mkataba huo, kulikuwa na tetesi kali zikimhusisha na Arsenal.
Vinicius Jr aizima ndoto ya Arsenal, asaini mkataba mpya na Real Madrid
Vinícius ameamua kubaki Santiago Bernabéu na kuendelea kuipigania Real Madrid. /

Vinícius Jr amefunga mjadala kuhusu hatma yake baada ya kusaini mkataba mpya wa miaka sita na Real Madrid.

Nyota huyo wa Brazil ameonyesha wazi kuwa bado ana imani na mradi wa Los Blancos, huku klabu hiyo ikiendelea kumchukulia kama mmoja wa wachezaji muhimu kwenye kikosi chao.

Mkataba huo mpya unamaanisha Vinícius ataendelea kuwatesa mabeki akiwa amevaa jezi nyeupe ya Madrid kwa miaka ijayo.

Kabla ya kusaini mkataba huo, kulikuwa na tetesi kali zikimhusisha na Arsenal, ambapo ilidaiwa kuwa miamba hiyo ya London ilikuwa inafuatilia kwa karibu hali ya mkataba wake.

Mashabiki walikuwa wameanza kuota ndoto za kumuona Emirates, lakini baada ya kusaini mkataba mpya, ndoto hizo zimezimika rasmi.