| Swahili
ULIMWENGU
2 dk kusoma
Meli ya China iliowekewa vikwazo na Marekani yapita Mlango Bahari wa Hormuz
Meli hiyo ya mafuta ni ya kwanza kupitia Mlango Bahari huo tangu Marekani ilipotangaza vikwazo kwa vigezo na mbinu za uwongo vyenye lengo la kuzuia meli kupita katika eneo hilo.
Meli ya China iliowekewa vikwazo na Marekani yapita Mlango Bahari wa Hormuz
Kilomita 39 za Mlango Bahari wa Hormuz ni eneo muhimu la njia ya mafuta, inayounganisha Ghuba na Ghuba ya Oman. / Reuters
tokea masaa 10

Meli ya mafuta inayomilikiwa na China na ambayo imewekewa vikwazo na Marekani imepita Mlango Bahari wa Hormuz, ikiwa ni ishara ya meli ya kwanza kupita katika njia hiyo ya kimkakati tangu vikwazo vilipowekwa.

Meli hiyo ya mafuta Rich Starry inamilikiwa na kampuni ya Shanghai Xuanrun Shipping, shirika lililo miongoni mwa waliowekewa vikwazo na Marekani. 

Data za kufuatilia usafiri wa baharini, zinaonesha meli hiyo ikivuka mlango bahari mapema siku ya Jumanne baada ya kuzunguka kizuizi Jumatatu jioni. Meli hiyo ilikuwa imeondoka Sharjah, UAE na sasa iko njiani kuelekea China.

Idara ya wizara ya ulinzi ya Marekani US CENTCOM ilisema siku ya Jumapili kuwa vizuizi "vitawekwa dhidi ya meli za mataifa yote bila upendeleo" zinazoingia na kutoka bandari za Iran katika Ghuba na Ghuba ya Oman. Muda mfupi baada ya hapo, Rais wa Marekani Donald Trump alisema meli za Iran zitakazokuja karibu na kizuizi hicho "zitashambuliwa mara moja.”

Mawasiliano ya uwongo kupenya kwenye kizuizi   

Katika tukio lingine, meli ya mafuta iliokuwa imetoka Kisiwa cha Iran cha Kharg Ilionekana katika mlango bahari huo siku ya Jumatatu ikitoa taarifa za uwongo, kuwa imeanza safari yake kutoka Saudi Arabia.

Mbinu kama hizo zinaendelea kutumika zaidi. Tangu kuanza kwa mzozo, meli kadhaa zimejaribu kuficha njia ya safari zao kwa kutoa taarifa za uwongo au kuzima mfumo wa ufuatiliaji wa safari za meli.

CHANZO:TRT World and Agencies