Nigeria kukopa dola bilioni $6 kutoka taasisi za kigeni

Wabunge wa Nigeria wameidhinisha ombi la Rais Bola Tinubu wa mikopo katika muda mfupi, kusababisha shutuma kutoka kwa baadhi ya wadau.

By
Rais wa Nigeria Bola Ahmed Tinubu alifanya ziara rasmi Uingereza mwezi uliopita ambapo alipata mkopo wa kukarabati bandari. / AP

Nigeria inatarajiwa kuomba mkopo wa dola bilioni $6 kutoka kwa taasisi na fedha za kigeni ili kukabiliana na changamoto za kiuchumi na miundombinu.

Mabunge yote mawili, yaliidhinisha ombi la Rais Bola Tinubu la kutaka kuomba mikopo kutoka kwa taasisi za kigeni siku ya Jumanne, Machi 31.

Taarifa za vyombo vya habari, vilieleza kuwa Rais Tinubu alitaka kuomba dola bilioni $5 kutoka kwa Benki ya First Abu Dhabi na nyingine dola bilioni $1 kutoka kwa taasisi ya Uingereza, UKEF.

Serikali ya Nigeria inasema kuwa sehemu kubwa ya fedha hizo itatumika kusaidia bajeti ya nchi ya dola bilioni $49.4 ya 2026, ambao pia uliidhinishwa na wabunge siku ya Jumanne, huku sehemu ya mikopo hiyo ikielekezwa katika ukarabati wa bandari mbili mjini Lagos.

Iliidhinishwa kwa muda mchache

Wabunge waliidhinisha mpango huo ndani ya saa chache ya kupokea ombi hilo kutoka kwa Rais Tinubu, kusababisha shutuma kutoka kwa baadhi ya wadau.

Aliyekuwa makamu wa raia na kiongozi wa upinzani Atiku Abubakar alieleza wasiwasi wake kuhusu athari za madeni kwa uchumi wa nchi, akisema maamuzi kama hayo hayatakiwi kuchangamkiwa na wabunge “bila kufuata utaratibu”.

Hata hivyo, serikali ya Nigeria imejitetea kuhusu mpango huo wa kuomba mabilioni kutoka taasisi za nje.