| Swahili
UTURUKI
2 dk kusoma
Rais Erdogan asema uhusiano wa Uturuki, Marekani lazima 'uimarike zaidi', vikwazo viondolewe
Rais wa Uturuki amepongeza uhusiano wao na Marekani, akisema kuwa ulinzi umekuwa moja ya maeneo ya msingi ya ushirikiano wa Uturuki na Marekani na Uturuki iko tayari kuuimarisha zaidi, katika maeneo kama nishati ya nyuklia na masuala ya anga.
Rais Erdogan asema uhusiano wa Uturuki, Marekani lazima 'uimarike zaidi', vikwazo viondolewe
Erdogan anasema Uturuki itaendelea kuimarisha nafasi yake kama "kisiwa thabiti" licha ya mizozo na migogoro inayowazunguka.

Uhusiano wa Uturuki na Marekani lazima "uimarike zaidi’’ kwa kuondoa vikwazo kati yao, Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan amesema.

"Tunataka kuimarisha uhusiano wetu kwa kuachana na vikwazo ambavyo havikutakiwa kuwepo kabisa kati ya washirika wawili," Erdogan alisema katika hafla moja jijini New York.

"Kuimarisha sekta ya ulinzi, ambayo imekuwa moja ya maeneo ya msingi ya ushirikiano wa Uturuki na Marekani, yote kwa mataifa hayo mawili na ndani ya NATO ni muhimu sana," alisema.

"Tuko tayari kuimarisha ushirikiano tulionao na Marekani katika maeneo ya nyuklia, nishati ikiwa ni pamoja na gesi, masuala ya anga na teknolojia ya hali ya juu," aliongeza.

"Kuimarisha zaidi ushirikiano wetu na Marekani kwa njia mbalimbali, ikiwemo fursa ya kushirikiana katika uzalishaji pamoja, itakuwa ni suala la maslahi ya kwetu sote," alisema.

Erdogan anasema makampuni ya Uturuki yamefikia viwango ambavyo vinayawezesha kuwekeza nchini Marekani, akieleza matumaini yake kuwa Uturuki hivi karibuni itakuwa miongoni mwa mataifa 10 bora yanayouza vifaa vya kijeshi nje ya nchi kote duniani.

"Natumai kuwa ushirikiano thabiti na muungano kati ya Uturuki na Marekani utaimarika zaidi katika karne ya pili ya uhusiano wetu wa kidiplomasia," alisema.

Erdogan pia alisema kuwa Uturuki itaendelea kuimarisha nafasi yake kama "kisiwa thabiti" licha ya mizozo na migogoro inayowazunguka.

'Sauti ya wanaonyanyaswa'

Erdogan atahutubia Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa siku ya Jumanne kwa mara ya 16.

Awali, Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Burhanettin Duran alisema sauti ya Uturuki na sauti ya busara itasikika tena kwenye jukwaa la Umoja wa Mataifa.

"Rais wetu kwa mara nyingine tena atazungumzia kuhusu haki kwenye hotuba ambayo itakuwa ni fahari kwa taifa letu, na atakuwa sauti ya wanaonyanyaswa, wale ambao sauti zao hazisikiki, na wale wanaosubiri haki itendeke," Duran alisema katika ujumbe kwenye mtandao wa kijamii wa Uturuki NSosyal.

"Atatoa wito wa haki—kutoka Gaza hadi kwa wanaonyanyaswa duniani - na busara kwa watu wote. Kwa sababu dunia inahitaji kuwa na haki, utawala wa sheria, na sauti za watu wanaotaka usawa ziko wazi. Ili tuwe na ulimwengu wa haki, Erdogan ndiyo sauti ya haki!"

CHANZO:TRT World