Mfanyabiashara mashuhuri wa Zimbabwe, Wicknell Chivayo, amefariki dunia baada ya helikopta binafsi aliyokuwa akisafiria pamoja na watu wengine watano kuanguka katika eneo la vijijini la Marondera, jioni ya Jumatano, 30 Septemba.
Msemaji wa familia, Herbert Chivayo, amethibitisha kifo cha Chivayo pamoja na mke wake, Lucy Muteke.
ZILIZOPENDEKEZWA
Akizungumza na Shirika la Habari la ZBC, Herbert amesema familia imekumbwa na huzuni kubwa.
Msemaji wa Polisi ya Zimbabwe, Kamishna Paul Nyathi, pia amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo, akisema helikopta hiyo ilikuwa na watu sita.
CHANZO:TRT Afrika and agencies
























