Na Evelyn Gitau
Huku dunia ikiadhimisha Siku ya Kimataifa ya Wanawake na Wasichana katika Sayansi, ni hatua muhimu kwa bara la Afrika kutafakari.
Hatua kama hizi siyo kwa ajili ya kusherehekea tu. Ni wito wa kutambua pale uwezo wa sayansi ulipo na nani anaufanyia kazi.
Kote barani Afrika, wanawake siyo wanaimarisha uvumbuzi wa kisayansi tu; wanaweka misingi yake, ukusanyaji wa data, mifumo ya usambazaji, na imani kwa umma kufanya sayansi iwe ya kuaminika na yenye mafanikio.
Uongozi huu unafanyika barani Afrika kwa makusudi kutoa muelekeo kwa mustakabali wa sayansi. Mkakati wa Umoja wa Afrika wa Sayansi, Teknolojia na uvumbuzi wa Afrika (STISA) 2034 unaweka sayansi siyo tu kama jambo zuri lakini kama kiungo muhimu cha kubadilisha mifumo ya kijamii ya kiuchumi.
Inaonesha hatua kutoka kuwa wapokeaji wa ubunifu hadi kuwa wamiliki wa ubunifu. Ilhali wakati mwingine mkakati unakuwa na uwezo sawa na watu waliopewa mamlaka ya kuuongoza.
Wanaosimamia uongozi huu, miongoni mai ni Allen Mukhwana, Mkuu wa Kuimarisha Miradi ya Kisayansi katika Wakfu wa Sayansi kwa Afrika, wanaotambua kuwa sayansi siyo tu kuhusu kinachoendelelea katika maabara lakini katika kuhakikisha inaaminika na kuwajibika katika mzunguko wa utafiti.
Katika dunia ambayo sampuli za kibayolojia na taarifa kuhusu afya zinatoa muelekeo wa uwezo wa kisayansi duniani, umuhimu wake siyo tu wa kawaida. Ni sehemu ya namna utaalamu unavyokusanywa, kusimamiwa, na kusambazwa.
Viongozi wanawake katika kuangazia masuala ya data wanatoa muelekeo wala siyo kutengwa, lakini kama ilivyo maadili, uwazi na ushirikiano duniani ni muhimu.
Afrika Magharibi, Iruka Okeke, Profesa katika Chuo Kikuu cha Ibadan nchini Nigeria, ni miongoni mwa walio mstari wa mbele katika juhudi za kukabiliana na suala muhimu zaidi barani Afrika.
Miradi ambayo wakati fulani iliimarisha kujumuishwa katrika sayansi, elimu, na uongozi katika utafiti sasa inatiliwa shaka, inapokonywa ufadhili, au inadumazwa kisiasa. For Africa, this shift is not a signal to retreat from equity agendas but a reminder of their strategic importance.
Sayansi haitoli muelekeo kwa jamii kupitia maabara pekee. Mawasiliano ya Kisayansi, hasa yanayoongozwa na wanawake, yenye kuunganisha uvumbuzi, maamuzi na uwajibikaji.
Nchini Kenya, waandishi walioshinda tuzo kama Hellen Shikanda na Angela Oketch wamejitahidi kuleta uwiano wa suala la utafiti na uhalisia wa maisha ya kila siku. Urithi wa marehemu Elizabeth Merab unaonesha namna gani uandishi wa masuala ya sayansi unaweza kutoa muelekeo halisi wa sera na ufahamu kwa umma.
Na wakati tukiondoka kwenye Siku ya Kimataifa ya Wanawawake na Wasichana katika Sayansi na kuelekea katika Siku ya Kimataifa ya Wanawake, swali siyo tena kama wanawake wa Afrika wanaweza kutoa muelekeo katika sayansi. Tayari wanaanya hivyo. Swali la msingi ni kama taasisi, wafadhili, na serikali ziko tayari kutambua uwekezaji wa muda mrefu, mamlaka za kufanya maamuzi, na uaminifu.
Mwandishi, Dkt Evelyn Gitau ni Mwanasayansi Mwandamizi wa Wakfu wa SFA, ambapo anaongoza idara ya sayansi na mikakati ya taasisi hiyo.
Kanusho: Maoni ya mwandishi hayahusiani na sera ya uhariri ya TRT Afrika.















