| Swahili
ULIMWENGU
2 dk kusoma
Ndege mpya ya Trump haina baadhi ya mifumo ya kujihami: Ripoti
Jeshi la Anga la Marekani limekiri kuwa ndege hiyo haina vifaa vyote vinavyohitajika kwenye Air Force One.
Ndege mpya ya Trump haina baadhi ya mifumo ya kujihami: Ripoti
Wataalamu wanaonya kuwa Boeing 747-8 aliyozawadiwa na Qatar inaweza kuongeza kiwango cha hatari katika safari za kimataifa. /

Ndege mpya ya Air Force One aliyotumia Rais Donald Trump kusafiria Uturuki haina baadhi ya mifumo ya kujihami iliyokuwepo kwenye ndege ya awali ya rais, ikiwemo uwezo wa hali ya juu wa kujikinga dhidi ya makombora, kwa mujibu wa ripoti ya gazeti la The New York Times iliyowanukuu maafisa wa Marekani.

Wataalamu wanaonya kuwa Boeing 747-8 aliyozawadiwa na Qatar inaweza kuongeza kiwango cha hatari katika safari za kimataifa, huku ripoti zikidai kuwa Walinzi Rasmi wa Viongozi Marekani walimshauri Trump kurudi Marekani kwa kutumia Air Force One ya zamani.

Ikulu ya White House ilitetea usalama wa ndege hiyo, lakini haikutoa maelezo kuhusu uwezo mahsusi. Msemaji wa Ikulu, Steven Cheung, alisema: "Air Force One mpya ni ndege ya kisasa yenye viwango vya juu vya usalama ambayo imewekewa mifumo madhubuti ya kulinda usalama wa rais na wafanyakazi wake."

Jeshi la Anga la Marekani limekiri kuwa ndege hiyo haina vifaa vyote vinavyohitajika kwenye Air Force One . Limeieleza kuwa ni ndege ya muda itakayotumika hadi ndege mbili mpya za rais zinazotengenezwa na Boeing zitakapokamilika.

Katika taarifa ya Juni 19, Jeshi la Anga lilisema: "Wamechukua tahadhari zote za kiusalama, ulinzi na mawasiliano ya misheni."

Hata hivyo, maafisa wanaofahamu mchakato wa maboresho ya ndege hiyo walisema haijapewa mifumo sawa ya kujihami dhidi ya mashambulizi kama ilivyokuwa kwa ndege ya awali, ingawa Jeshi la Anga halijabainisha ni mifumo gani hasa iliyoachwa.

Maafisa wawili wa zamani wa Jeshi la Anga waliokuwa sehemu ya mpango wa kubadilisha ndege ya rais walisema walishangazwa na uamuzi wa Trump kuitumia ndege hiyo katika safari ya nje ya nchi, wakieleza kuwa mazingira ya usalama katika safari hizo huwa na hatari kubwa zaidi.

Waliongeza kuwa kasi ya maandalizi huenda haikuruhusu muda wa kutosha wa kufunga mifumo yote ya usalama ambayo kwa kawaida hupatikana kwenye Air Force One iliyokamilika.

 

 

CHANZO:AA
Soma zaidi
Ukraine, Uholanzi zatiliana saini mkataba wa ulinzi wakati wa mkutano wa NATO
Gaza yavunja utawala kabla ya uhamisho wa mamlaka chini ya makubaliano ya kusitisha mapigano
Ufaransa yakumbwa na wizi mwingine mkubwa wa vito vya thamani kutoka jumba la makumbusho
Trump kukutana na Zelenskyy, Sharaa wa Syria wakati wa mkutano wa NATO mjini Ankara
Watu 8 wauawa katika tukio la hivi punde la uhalifu wa  bunduki nchini Marekani.
Maombi yamefanyika kwa ajili ya Khamenei wa Iran katika siku ya pili ya sherehe za mazishi
Sherehe za mazishi ya Ali Khamenei zinaanza nchini Iran huku umati mkubwa ukidai kulipizwa kisasi
Uturuki yakanusha taarifa za kupotosha kuhusu tishio la shambulio wakati wa mkutano wa NATO
Waziri Mkuu wa Moldova ajiuzulu baada ya miezi nane madarakani
Kanisa Katoliki lajitenga na Jumuiya ya Mtakatifu Pius wa 10
Mazungumzo ya nyuklia kati ya Iran na Marekani yamepiga hatua nzuri: Trump
Jinsi urembeshaji wa kitamaduni unavyoweka utambulisho wa Wapalestina hai katika diaspora
Ufaransa yarekodi vifo zaidi ya 1,000 katika siku tano huku wimbi la joto likizidi kupanda
Kisa cha paka Larry na Mawaziri Wakuu wa Uingereza
Huduma za usafirishaji zapungua Mlango Bahari wa Hormuz baada ya mashambulizi ya meli za mizigo
Ajali mbaya ya ndege nchini Ufaransa, uchunguzi waanza
Umoja wa Mataifa unakadiria karibu watu milioni 6.8 waliathiriwa na tetemeko la ardhi la Venezuela
Lebanon, Israel na Marekani watia saini mpango wa makubaliano ya amani
Rais Zelenskyy  wa Ukraine ‘atenga’ siku 40 za kuishambulia Urusi
Klabu ya 1860 Munich ya nchini Ujerumani yaelekea kufilisika