21 Novemba 2025
Shirika la Uturuki la TİKA limeimarisha uwezo wa Kitivo cha Matibabua cha Chuo Kikuu cha Kiislamu Uganda kwa mafunzo na utafiti kwa kuwapa vifaa vya kisasa vya maabara kwa maabara yao ya bayolojia na dawa.
ZILIZOPENDEKEZWA
Hafla hiyo ilihudhuriwa na Waziri wa Ulinzi wa Uganda, Huda Abason Oleru, na Mehmet Fatih Ak, Balozi wa Uturuki nchini Uganda.
Ndani ya mpango huo, TİKA imechangia katika kutoa vifaa vya kisasa kwa maabara ikiwemo makabati ya maabara, mashine ya kusafisha vifaa, sehemu ya kuhifadhi damu, mashine ya kutathmini vipimo na vifaa vingine muhimu vya kufanya utafiti mahsusi wa kisayansi.
CHANZO:TRT Afrika Swahili



















