Athari za Iran kufunga Mlango Bahari wa Hormuz
ULIMWENGU
3 dk kusoma
Athari za Iran kufunga Mlango Bahari wa HormuzIran ilitangaza kufungwa rasmi kwa njia ya maji iliyo kati yake na Oman ambapo zaidi ya mapipa milioni 20 ya mafuta husafirishwa kila siku na meli kupitia eneo hilo.
Mlango bahari wa Hormuz Ina upana wa takriban kilomita 33 katika sehemu yake nyembamba zaidi / Reuters
tokea saa limoja

Vita vinavyoratibiwa na Israel na Marekani dhidi Iran vilivyoanza Februari 28, 2026 tayari zimeanza kuathiri biashara ya kimataifa.

Iran ilitangaza kufungwa rasmi kwa njia ya maji iliyo kati yake na Oman ambapo zaidi ya mapipa milioni 20 ya mafuta husafirishwa kila siku na meli kupitia eneo hilo.

Unaitwa Mlango Bahari wa Hormuz.

Una upana wa takriban kilomita 33 katika sehemu yake nyembamba zaidi, na njia ya usafirishaji ni 3km tu kwa upana katika pande zote mbili.

Lakini karibu thuluthi moja ya jumla ya matumizi ya mafuta duniani hupitia katika eneo hili kila siku.

Na sasa kulingana na takwimu za usafirishaji mamia ya meli za mafuta zimeng'oa nanga kwenye maji ya Ghuba nje ya Mlango-Bahari wa Hormuz na baadhi tayari kuanza safari kwa kutumia njia ndefu zaidi.

Wamiliki wa meli walipokea onyo iliyotolewa na Iran kwamba eneo hilo kuanza sasa limefungwa. Huku taarifa zikionesha tayari kuna baadhi ya meli za mafuta zimeshambuliwa kwa kukiuka amri hiyo.

Nchi nyingi za Kiarabu ambazo ndio wazalishaji wakubwa wa mafuta duniani, kama vile Iran yenyewe, Iraq, Kuwait, Qatar, Saudi Arabia na  UAE hutumia mlango huo.

Wanunuzi wake ni China, India, Japan, na Korea Kusini. India, ikiwa nchi hizi zinaagiza karibu nusu ya mafuta yake ghafi kupitia barabara hii ya meli.

Kwa kuongeza, theluthi moja ya biashara ya mbolea duniani hupitia mlango huu wa bahari. Usambazaji wa bei ya nishati na kilimo tayari imeyumbishwa na vita vya Urusi na Ukraine.

Je, dunia nzima ikiwemo Afrika itaathiriwa vipi na kufungwa kwa njia hiyo?

Nchi ambazo zinategemea kupokea mafuta na gesi pia ni muhimu katika uzalishaji wa bidhaa zinazotumwa duniani kote ikiwemo Afrika.

Wanapotafuta njia mbadala, hii inaweza kuwa na athari katika kucheleweshwa kwa uzalishaji wa bidhaa na vile vile kupanda kwa bei ya bidhaa zinazotumiwa na kusafirishwa kutoka Afrika.

Mafuta na gesi yanauzwa kimataifa. Kwa hivyo hata nchi ambazo mahitaji yao ya nishati hayatimizwi na uagizaji kutoka Ghuba ya Uajemi zitaathiriwa na ongezeko la bei.

Wataalamu wanasema bei ya mafuta inatarajiwa kuongezeka hadi $100.

Hii inaweza pia kumaanisha kuwa sasa utalipa zaidi kwa usafiri wa ndege kwani gharama za usafiri jumla zinaongezeka.

Kwa wale wanaotegemea kusafirisha mizigo kupitia baharini, bila shaka watalipa zaidi na watalazimika kuvumilia kwani meli za mizigo sasa zitatumia njia ndefu zaidi hadi Hormuz itakapofunguliwa.

Bima nayo ya mizigo itaongezeka kwa sababu meli sasa zitakuwa zinapita katika njia ambazo ni ndefu na hatari zaidi.

Barabara ya Hormuz ni muhimu sana kwa sababu hakuna mbadala mwepesi, kwa sababu pia ni njia pekee ya maji yenye kina kirefu kwa meli kubwa zaidi za mafuta duniani.

Iran kihistoria imekuwa ikitishia kuufunga Mlango wa Bahari wa Hormuz lakini haijawahi kufanya hivyo.

Mnamo 2025 ilifikiria kuufunga huo baada ya Marekani  kushambulia vituo vyake vya nyuklia lakini haikufanya hivyo. Lakini sasa imekuwa sio tishio tena, bali ni uhalisia kutokana na yanayojiri.

CHANZO:TRT Swahili