Uturuki imelaani vikali shambulio la kigaidi katika jimbo la Kwara nchini Nigeria ambalo lilisababisha vifo vya takriban watu 170.
"Tumehuzunishwa sana na vifo viliyosababishwa na shambulio la kigaidi lililotokea katika jimbo la Kwara nchini Nigeria," Wizara ya Mambo ya Nje ya Uturuki iliandika kwenye mtandao wa kijamii wa X siku ya Alhamisi.
Wizara hiyo ilituma salamu za rambirambi kwa familia za walio poteza maidha na watu wa Nigeria, ikithibitisha tena mshikamano wa Uturuki na nchi hiyo, na kuongeza kuwa "Uturuki itaendelea kuiunga mkono Nigeria katika mapambano yake dhidi ya ugaidi."
Siku ya Jumanne, makundi yenye silaha yalishambulia Jimbo la Kwara nchini Nigeria na kuua takriban watu 170.
Jimbo la Kwara, hasa jamii zilizo karibu na maeneo ya misitu, katika miezi ya hivi karibuni limekumbwa na matishio yanayoongezeka ya usalama yanayohusiana na ujambazi, utekaji nyara, na kuongozeka kwa makundi yenye silaha yanayotoroka operesheni za kijeshi katika majimbo jirani ya kaskazini-magharibi na kaskazini- ya kati.

















