| Swahili
AFRIKA
2 dk kusoma
Uturuki, Kenya yatia saini makubaliano ya ushirikiano wa ulinzi katika maonesho ya Istanbul expo
Mawaziri hao wa ulinzi walikutana katika maonesho ya sekta ya ulinzi ya SAHA 2026.
Uturuki, Kenya yatia saini makubaliano ya ushirikiano wa  ulinzi katika maonesho ya Istanbul expo
Waziri wa Ulinzi wa Uturuki Yasar Guler amekutana na Waziri wa Ulinzi wa Kenya Roselinda Soipan Tuya katika maonesho hayo. / AA

Uturuki na Kenya wametia saini makubaliano ya ushirikiano katika masuala ya ulinzi siku ya Jumatano wakiwa katika Maonesho ya Kimataifa ya Ulinzi na Anga ya SAHA 2026 jijini Istanbul.

Waziri wa Ulinzi wa Uturuki Yasar Guler amekutana na Waziri wa Ulinzi wa Kenya Roselinda Soipan Tuya katika maonesho hayo, ambapo Anadolu ni mshirika wa mawasiliano ulimwenguni.

Kufuatia mkutano wao katika ukumbi wa Istanbul Expo, mawaziri hao wawili walitia saini makubaliano yanayolenga kuimarisha ushirikiano wa masuala ya ulinzi kati ya mataifa hayo mawili.

SAHA 2026, inayoandaliwa na SAHA Istanbul, inaleta pamoja makampuni ya ulinzi na anga, maafisa wa manunuzi, wajumbe wa kijeshi, na wawakilishi wa sekta ya ulinzi kutoka Uturuki na nje.

Mauzo ya nje ya Uturuki ya sekta ya ulinzi na anga yaongezeka kwa asilimia 28%

Wakati huohuo, mauzo ya nje ya Uturuki na anga katika miezi minne ya kwanza ya mwaka yameongezeka kwa Dola bilioni $2.8, kufikia asilimia 28% yakilinganishwa na kipindi kama hicho mwaka uliopita, waziri wa biashara wa Uturuki alisema Jumatano.

Akizungumza na waandishi wa habari katika maonesho ya Kimataifa ya sekta ya Ulinzi na Anga SAHA 2026 jijini Istanbul, Omer Bolat alisema mauzo ya nje ya sekta ya ulinzi na anga ya Uturuki yameongezeka kutoka Dola milioni $248 katika kipindi cha miongo miwili iliopita hadi Dola bilioni $10.05 mwaka jana pekee.

“Mwaka huu, tumekuwa na ongezeko la asilimia 28% katika miezi minne ya kwanza. Mauzo ya dola bilioni $2.8,” Bolat alisema, akiongeza kuwa mwaka uliopita sekta hiyo ilipita kiasi cha Dola bilioni $10 kwa mauzo ya nje kwa mara ya kwanza.

Maonesho hayo, yaliyoandaliwa na SAHA Istanbul -- muungano mkubwa wa sekta ya ulinzi, safari za ndege na anga Uturuki na Ulaya -- yanafanyika huku Anadolu ikiwa mshirika wa mawasiliano kote ulimwenguni. Yanaendelea hadi Jumamosi.

CHANZO:AA