| Swahili
AFRIKA
1 dk kusoma
Wakimbizi wa DRC waliokuwa Burundi warejea makwao
Kulingana na UNHCR, Burundi inahifadhi zaidi ya wakimbizi 200,000 kutoka DRC, wakiwemo wengine 66,000 walioko katika kambi ya Busuma.
Wakimbizi wa DRC waliokuwa Burundi warejea makwao
Mchakato wa kurejea nyumbani, ulisimamiwa na mwakilishi wa ubalozi wa DRC nchini Burundi./Picha:@RTNBurundi

Maelfu ya wakimbizi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) wamerejea makwao, wakitokea Burundi.

Wakimbizi wapatao 470 walikuwa ni sehemu ya kundi la mwisho kurudi makwao, baada ya kukimbia machafuko katika eneo la Uvira, miezi minne iliyopita.

Watu hao, wlaikuwa hifadhi katika kambi ya Busuma iliyoko katika eneo la Buhumuza nchini Burundi.

Kufikia mwezi Machi mwaka huu, wakimbizi takriban 33,000, walirejea makwao, kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa.

Kikundi cha waasi cha M23 ambacho kilikuwa kimetwaa maeneo ya Kaskazini na Kusini mwa Kivu, yameanza kuondoka katika eneo la Uvira, kufuatia shinikizo la kimataifa.

Mchakato wa kurejea nyumbani, ulisimamiwa na mwakilishi wa ubalozi wa DRC nchini Burundi.

Kulingana na Kamishna wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR), zoezi hilo linatarajiwa kudumu kwa muda wa wiki kadhaa.

Kwa mujibu wa UNHCR, Burundi inahifadhi zaidi ya wakimbizi 200,000 kutoka DRC, wakiwemo wengine 66,000 walioko katika kambi ya Busuma.