Uturuki haitakubali uchokozi katika eneo la Mediterania ya Mashariki: Rais Erdogan
Uturuki inafuatilia kwa karibu ongezeko la uchokozi na vitisho dhidi ya maslahi ya nchi hiyo pamoja na maslahi ya Waturuki wa Kupro (Turkish Cypriots) katika Mediterania ya Mashariki, amesema kiongozi wa Uturuki.
Uturuki haiwezi kulazimishwa, au kuruhusu uharamia na ujangili katika eneo lake la baharini, amesema Rais Recep Tayyip Erdogan.
Katika ujumbe wa mwaka mpya, Erdogan alisema siku ya Jumatano kuwa Ankara inafuatilia kwa makini ongezeko la uchokozi na vitisho vinavyolenga maslahi ya Uturuki na yale ya Waturuki wa katika eneo la Mediterania ya Mashariki.
“Kadiri amani inavyozidi kuimarika nchini Syria, idadi ya Wasyria wanorudi kwao kwa hiari imeongezeka,” alisema Erdogan, akibainisha kuwa Wasyria 600,000 wamerejea nchini mwao katika mwaka uliopita.
Alisisitiza kuwa Uturuki itaunga mkono utawala mpya wa Syria ili kuhakikisha usalama na utulivu kwa Wasyria wote, bila kujali kabila au madhehebu yao.
Kuhusu suala la Gaza, Erdogan alisema Uturuki haitanyamaza hadi wale waliohusika na vifo vya Wapalestina 71,000—wengi wao wakiwa wanawake na watoto—wawajibishwe.
Rais huyo wa Uturuki aliongeza kuwa Ankara inafanya kazi kwa bidii kuhakikisha Israel inasitisha mashambulizi, inaharakisha uingizaji wa misaada ya kibinadamu kwenda Gaza, na inaruhusu juhudi za ujenzi kuanza.