| Swahili
ULIMWENGU
1 dk kusoma
Kiongozi wa mapinduzi ya Myanmar ashinda kiti cha Urais
Hlaing anakumbukwa kwa kumuondoa madarakani Aung San Suu Kyi katika mapinduzi ya mwaka 2021.
Kiongozi wa mapinduzi ya Myanmar ashinda kiti cha Urais
Hlaing anakumbukwa kwa kumuondoa madarakani Aung San Suu Kyi katika mapinduzi ya mwaka 2021./Picha:Wengine
tokea masaa 4

Kiongozi wa zamani wa kijeshi wa Burma, Min Aung Hlaing ameshinda kiti cha Urais wa nchi hiyo baada ya kuchaguliwa siku ya Ijumaa.

Wabunge wa nchi hiyo walimchagua Hlaing kwa kura 429, kulingana na shirika la habari la Xinhua.

Akiongoza mapinduzi ya kijeshi ya mwaka 2021, Hlaing alihudumu kama Amiri Jeshi Mkuu, kabla ya kuachia nafasi hiyo mwezi Machi mwaka huu, na kugombea nafasi ya Urais.

Hlaing anakumbukwa kwa kumuondoa madarakani Aung San Suu Kyi katika mapinduzi ya mwaka 2021.

Wakati wa utawala wake kama kiongozi wa kijeshi, Myanmar ilikosolewa kimataifa kwa mauaji ya watu wa jamii ya Rohingya.

Novemba 2024, Mwendesha Mashitaka wa ICC, Karim Khan alitoa kibali cha kukamatwa kwa Hlaing, akidai kuwa kuna kila sababu za kumuhusisha yeye na uhalifu dhidi ya binadamu, ikiwemo mateso ya watu wa jamii ya Rohingya.