| Swahili
AFRIKA
1 dk kusoma
Kenya yaidhinisha kituo cha Marekani kwa karantini ya Ebola kutokana na mlipuko DRC, afisa asema
Kenya imeidhinisha mpango wa Marekani wa kufungua kituo cha karantini cha Ebola, afisa wa Marekani amesema
Kenya yaidhinisha kituo cha Marekani kwa karantini ya Ebola kutokana na mlipuko DRC, afisa asema
Idhini ya Kenya inawapa Marekani ruhusa ya kutua katika kambi ya jeshi la anga Laikipia katikati mwa Kenya. / Reuters

Kenya imetoa idhini kwa maandishi kwa ajili ya kufunguliwa kwa kituo cha karantini katika taifa hilo la Afrika Mashariki kwa Wamarekani waliotangamana na watu walioambukizwa Ebola Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kwenye mlipuko huo, maafisa wawili wa Marekani wameiambia Reuters.

Idhini hiyo inawapa Marekani fursa ya kutua katika kambi ya jeshi la anga eneo la Laikipia katikati mwa Kenya, mmoja wa maafisa hao amesema.

Maafisa wa wizara za mambo ya nje na afya hawakupatikana kutoa ufafanuzi kuhusu suala hilo.

Kenya imekuwa ikitaka kituo hicho kiwepo kwa raia wa mataifa yote, siyo kwa Marekani pekee. Haikufahamika mara moja kama mpango utakuwa huo.

Kituo hicho kitasimamiwa na maafisa wa afya wa Marekani.

Katika taarifa siku ya Jumatano, wizara ya afya ya Kenya ilisema inajadiliana na Marekani na washirika wengine duniani kuhusu kushirikiana katika kukabiliana na Ebola lakini haikutaja mipango ya kituo cha karantini.

Daktari mmoja Mmarekani aliyeambukizwa Ebola na raia wengine wa Marekani waliotangamana na watu waliokuwa na virusi walipelekwa Ujerumani kwa matibabu na uangalizi. Daktari mwingine Mmarekani aliyetangamana na watu wenye virusi alisafirishwa hadi Jamhuri ya Czech.

CHANZO:TRT Afrika Swahili