| Swahili
UTURUKI
3 dk kusoma
Sabiha Gokcen ya Istanbul yaongoza kwa ukuaji wa idadi ya abiria kati ya viwanja vya ndege Ulaya
Uwanja huo umeimarika zaidi katika viwango vya abiria miongoni mwa viwanja vikubwa Ulaya kipindi cha nusu ya kwanza ya mwaka 2026, kulingana na Baraza la Viwanja vya Ndege vya Kimataifa la Ulaya (ACI).
Sabiha Gokcen ya Istanbul yaongoza kwa ukuaji wa idadi ya abiria kati ya viwanja vya ndege Ulaya
(MAKTABA) Uwanja wa Ndege wa Sabiha Gokcen uliwahi kutangazwa uwanja unazingatia muda zaidi barani Ulaya. / Anadolu Agency

Uwanja wa Kimataifa wa Sabiha Gokcen wa Istanbul umeimarika zaidi katika viwango vya abiria miongoni mwa viwanja vikubwa Ulaya kipindi cha nusu ya kwanza ya mwaka 2026, kulingana na Baraza la Viwanja vya Ndege vya Kimataifa la Ulaya (ACI).

Idadi ya abiria katika uwanja wa Sabiha Gokcen iliongezeka kwa asilimia 6.4 ikilinganishwa na kipindi kama hicho mwaka jana, kuufanya kuwa uwanja unaokuwa kwa kasi miongoni mwa Viwanja Vikubwa vya Ndege, ikiwa inajumuisha viwanja vinavyohudumia abiria zaidi ya milioni 40 kila mwaka.

Uwanja huo ulihudumia abiria milioni 23.6 katika miezi sita ya kwanza ya mwaka 2026, kufanya kuwa ongezeko la asilimia 7.1 katika kipindi kama hicho mwaka uliopita.

Uwanja huo umeshinda viwanja vingine vikubwa barani Ulaya, ikiwemo Barcelona (ongezeko la asilimia 4.4), Madrid (asilimia 4.2) na Rome Fiumicino (asilima 0.3).

Shinikizo za kisiasa zinadumaza ukuaji kwa ujumla

Kuimarika kwa Sabiha Gokcen pia kumezidi wastani wa Ulaya. Idadi ya abiria katika viwanja vya ndege kote barani Ulaya iliongezeka kwa asilimia 2.6 katika kipindi cha miezi sita ya kwanza ya mwaka, huku ukuaji ukipungua kutoka kwa asilimia 4.3 robo ya kwanza hadi asilimia 1.3 robo ya pili.

ACI Europe imeeleza kuwa kupungua kwa sehemu fulani ni kutokana na vita vya Mashariki ya Kati, ambavyo vilipunguza idadi ya abiria katika kanda hiyo na kufanya baadhi ya mashirika ya ndege kupunguza idadi kutokana na kupanda kwa bei ya mafuta kulikosababisha kuongeza gharama za uendeshaji.

Viwanja vya ndege vya Uturuki vilipata idadi zaidi ya abiria kwa asilimia 2.8 katika kipindi cha nusu ya kwanza ya mwaka, ikiwa ni zaidi kidogo ya wastani wa Ulaya.

Licha ya ukuaji mdogo barani Ulaya, ACI Europe inasema Uturuki inaendelea kuwa moja ya soko la sekta ya usafiri wa ndege inayokuwa kwa kasi.

Miongoni mwa viwanja vya ndege vyenye shughuli nyingi barani Ulaya, Heathrow ya London inabaki kuwa uwanja wa ndege mkubwa ukihudumia abiria milioni 40 kipindi cha nusu ya kwanza ya mwaka, ukifuatwa kwa karibu na Uwanja wa Ndege wa Istanbul ukiwa na idadi ya abiria milioni 39.84.

Siasa za dunia zinaathiri usafiri wa ndege

Mkurugenzi Mkuu wa ACI Europe Olivier Jankovec anasema yanayoendelea katika siasa za dunia kunaathiri zaidi usafiri wa ndege mwaka 2026, lakini bado watu wanaendelea kutumia usafiri huo.

"Ni wazi kuwa siasa za dunia zitaendelea kuathiri usafiri wa ndege mwaka huu," Jankovec amesema.

Aliongeza kuwa abiria barani Ulaya wanaendelea kutumia usafiri huo licha ya shinikizo kwa upatikanaji wa bidhaa za msingi na idadi ya wasafiri kutoka Marekani ya Kaskazini wanaongezeka msimu huu wa joto.

Kulingana na ripoti, idadi ya usafiri wa ndani barani Ulaya iliongezeka kwa asilimia 3 kipindi cha nusu ya kwanza ya mwaka, kushinda usafiri wa kimataifa, ambao uliongezeka kwa asilimia 2.5.

Iliashiria mara ya kwanza tangu sekta ya usafiri wa anga ilivyoimarika kutoka kipindi cha maambukizi ya COVID-19 kwamba usafiri wa ndani umekuwa zaidi kuliko usafiri wa kimataifa.

CHANZO:TRT World