| Swahili
UTURUKI
6 dk kusoma
Uturuki na India waweke 'tofauti zao kando' na kuangazia agenda chanya: Fidan
Waziri wa mambo ya nje wa Uturuki ameitaka India kuweka tofauti zao kando na kuangazia maeneo ya maslahi ya pamoja, huku mwanadiplomasia mwandamizi wa India Talmiz Ahmad akisema kuwa mazungumzo ya hivi karibuni yanaashiria kuimarika kwa uhusiano.
Uturuki na India waweke 'tofauti zao kando' na kuangazia agenda chanya: Fidan
Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki Hakan Fidan akihutubia mkutano wa IISS Singapore Juni 2, 2026. / Reuters

Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki Hakan Fidan ametoa wito wa kuimarishwa kwa uhusiano kati ya Uturuki na India, akieleza kuwa tofauti kutokana na uhusiano wa karibu wa Uturuki na hazitakiwi kuzuia ushirikiano kati ya nchi hizo mbili zenye uwezo katika kanda.

Akizungumza katika ukumbi wa hafla ya 6 ya IISS Raffles nchini Singapore wiki iliopita, Fidan alisema Uturuki na India hawana malumbano makubwa na wana kila sababu ya kuwa na uhusiano mzuri.

"Tungependa kuwa na uhusiano mzuri zaidi na India. Hatuna mpaka wowote na India na hatuna suala lolote ambalo linafanya tuwe na matatizo na India," Fidan alisema wakati wa kipindi cha maswali na majibu baada ya hotuba yake hiyo. Alieleza kuwa Uturuki na India hawana historia ya mapigano na badala yake "kuna kila sababu ya kuwa na uhusiano mzuri."

Waziri wa mambo ya nje wa Uturuki alitetea uhusiano wa muda mrefu kati ya Uturuki na Pakistan, akiueleza kuwa wa kihistoria, huku akisisitiza kuwa uhusiano kama huo hautakiwi kuonekana kama kikwazo kwa ushirikiano na India.

"Uturuki siyo nchi pekee yenye uhusiano mzuri na wa kihistoria na Pakitsan katika baadhi ya masuala," Fidan alisema.

Akieleza uhusiano wa Uturuki na mataifa yenye uwezo duniani, Fidan amesema nchi zinatakiwa ziweke tofauti katika makundi mbalimbali na kuendelea kuangazia maeneo yenye maslahi ya pamoja.

"Kwa mfano, tofauti yetu na Urusi katika baadhi ya masuala, na Marekani katika baadhi ya mambo, nchi za Ulaya kati masuala fulani, lakini tunaweza kutofautisha suala moja na lingine," alisema.

"Kwa hiyo tunaweza kuweka tofauti zingine kando, kwenye mabano, na tuangazie agenda chanya."

Fidan alisema mtazamo kama huo unatakiwa kuwa muongozo wa uhusiano kati ya Uturuki na India.  "Nadhani hiki ndicho kinachotakiwa kufanyika kati ya Uturuki na India kwa sababu tunaweza kushirikiana katika mambo mengi, tunaweza kufaidi, na tunaweza kufuata njia hiyo," alisema.

Uhusiano kati ya India na Uturuki ulifikia kipindi kigumu kufuatia vita vya siku nne katia ya India na Pakistan Mei 2025. India ilikasirishwa na Uturuki kushtumu mashambulizi ya Indua na kudhihirisha kuunga mkono Pakistan wakati wa mzozo huo.

Ni muhimu kufahamu kuwa Uturuki ilikuwa miongoni mwa mataifa ya kwaza kushtumu mashambulizi ya kigaidi katika eneo la Pahalgam linalosimamiwa na India sehemu ya Kashmir Aprili 22, 2025, ambayo baadaye yalisababisha vita. Wizara ya Mambo ya Nje ya Uturuki ilitoa taarifa siku hiyo hiyo, ikiyataja mashambulizi kuwa “ya kikatili.”

Hata hivyo, kufuatia mashambulizi ya India ya Mei 6, 2025, ambayo yalilenga miundombinu nchini Pakistan, Uturuki ilishtumu hatua za India na kuunga mkono wito wa Pakistan wa kutaka uchunguzi ufanyike kwa shambulizi la kigaidi la Aprili 22.

Kuanzishwa kwa ushirikiano wa kidiplomasia

Matamshi ya hivi karibuni ya Fidan yanakuja huku kukiwa na dalili za kuanzishwa tena ushirikiano wa kidiplomasia kati ya nchi hizo mbili baada ya matukio ya kutoelewana mwaka uliopita.

Mwezi Aprili, India ilimualika Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki Berris Ekinci kwa mashauriano ya mkutano wa raundi ya 12 kati ya India na Uturuki ya Wizara ya Mambo ya Nje jijini New Delhi, ikiwa ni ya kwanza katika kipindi cha miaka minne.

Mwanadiplomasia mwandamizi wa India Talmiz Ahmad, balozi wa zamani nchini Saudi Arabia, Oman na UAE, anasema matamshi ya Fidan na yanayojiri hivi karibuni ni dalili nzuri za uhusiano wa Uturuki na India. 

"Inaonekana kuna utashi kutoka pande zote mbili kujaribu kusahau yaliyopita na kuona namna gani uhusiano huo unaweza kuanzishwa tena," alisema.

Maslahi ya pamoja

Licha ya tofauti za kisiasa katika baadhi ya masuala, Ahmad anaeleza kuwa Uturuki na India wana masuala mengi ya maslahi ya pamoja na uhusiano wa nchi hizo mbili una maeneo mengi ambayo yanaweza kuimarishwa.

"Binafsi naamini kuwa, kuna mengi tunaweza pamoja," alisema, akieleza kuhusu uwezo wa Uturuki katika uimarishaji wa miundombinu, viwanda, nishari na uchukuzi.

"Uturuki ni mdau mkubwa katika sekta ya miundombinu. Ni viongozi wa dunia. Wana uzoefu kuhusu suala la nishati na biashara. Nadhani masuala ya nishati yatakuwa muhimu sana."

Ahmad pia alieleza kuhusu umuhimu wa kimkakati wa majadiliano kati ya Uturuki na India huku hali ya usalama ikitatizwa kote Magharibi mwa Asia.

"Kama nchi mbili kubwa ambazo zinaathirika na yanayotokea Magharibi mwa Asia, India na Uturuki zinatakiwa kuwa na maelewano," alisema. "Hatuwezi daima kuelewana, lakini lazima tujadiliane."

Zaidi ya masuala ya kimkakati na kiuchumi, Uturuki na India wamekuwa na uhusiano thabiti wa kitamaduni. Katika miaka ya hivi karibuni, Uturuki imekuwa sehemu maarufu kwa watalii kutoka India na eneo zuri kwa harusi za kifahari za watu kutoka India, hasa jijini Istanbul na katika maeneo ya kupendeza ya pwani ya Mediterania.

Muunganiko huo umeimarishwa zaidi kupitia sekta ya burudani. Baadhi ya sinema za Bollywood zimerekodiwa nchini Uturuki katika kipindi cha muongo mmoja uliopita, kuwapa taswira watazamaji wa India kuhusu mandhari za nchi hiyo, utamaduni na urithi wa kihistoria. Tamthilia za televisheni za Uturuki pia zimekuwa maarufu katika baadhi ya maeno nchini India, kuchangia pakubwa kuhusu uwiano wa tamaduni za jamii hizo mbilo.

Mmoja wa mifano muhimu ni ziara ya nyota wa Bollywood Aamir Khan nchini Uturuki 2017 na 2020, ambapo watu wengi kutoka nchi zote mbili walifurahia na kuonesha msisitizo wa maelewano ya kitamaduni.

Jukumu la majukwaa mbalimbali

Mbali na uhusiano wa mataifa mawili, Ahmad anasema majukwaa mbalimbali yanaweza kutoa fursa zaidi kwa ushirikiano kati ya nchi hizo mbili.

Akizungumzia majukwaa kama BRICS na SCO, alieleza kuwa nchi zinaweza kuweka kando tofauti za mataifa mawili pale maslahi ya kimkakati yanapokuwa yanawiana.

"Naam, wakati mwingine kuna tofauti kati ya washirika katika majukwaa mbalimbali, lakini kama yale mazuri yanaweza kutoka katika baadhi ya majukwaa ambayo yatafunika tofauti hizo, basi nadhani tutasonga mbele," alisema.

Aliongeza kuwa ushirikiano wa karibu kati ya India na Uturuki utafaidi mashirika yote mawili, akieleza kuwa nchi hizo mbili ni wadau wakubwa katika kanda ambapo ushirikiano wao unaweza kuimarisha juhudi za majukwaa mbalimbali na majadiliano kwa nchi ambao zinakuwa kiuchumi.

Kwa upande wake, Fidan tayari ameshaeleza kuwa Uturuki haina matatizo na India na kuitaka India isitizame uhusiano wa Uturuki kwa jicho la ushirikiano na Pakistan pekee.

"Kama nilivyosema, hatuna tatizo kuhusu uhusiano wetu na India, na tunaomba India wasiwe na mtazamo tofauti kuhusu suala hili," Fidan alisema akiwa Singapore.

Ahmad alieleza kuwa kutoka na yanayojiri sasa hivi katika ngazi ya kidiplomasia, India inatarajiwa kuchukua hatua zenye tija. "Kama hilo litafanyika kweli, utaona India ikichukua hatua madhubuti zaidi."

Kwa sasa, wote Uturuki na India wanaonekana kuonesha kuwa pamoja na kuwepo kwa tofauti chache, majadiliano na ushirikiano wa kweli lazima yaendelee. 

Na kama anavyosema Fidan, changamoto ni kuweka tofauti zao "kando" na kuangazia fursa pana zilizopo kati ya mataifa hayo mawili yenye uwezo duniani.

CHANZO:TRT World
Soma zaidi
Spika wa bunge la Uturuki ashtumu UN kutokuwa 'thabiti' katika kuzuia migogoro
Waziri wa mambo ya nje wa Uturuki Hakan Fidan awasili Indonesia ili kuimarisha uhusiano wa kibiashar
Uturuki yatangaza timu ya wachezaji 26 kwa ajili ya Kombe la Dunia la FIFA 2026
Usambazaji wa gesi wa Uturuki, Azerbaijan nchini Syria kutasaidia maendeleo, usalama: Rais Erdogan
Mfumo wa kizazi kijacho wa Uturuki wa BLUEVISION waboresha usalama wa usafiri wa baharini
Erdogan aadhimisha kumbukumbu ya miaka 573 ya ushindi wa Istanbul, anatoa heshima kwa Mehmed II
Uturuki yawakumbuka waliouawa kwenye mashambulizi ya ubaguzi wa rangi ya Solingen 1993
Erdogan aadhimisha Eid al-Adha na ujumbe wa mshikamano wa Gaza, amkemea 'mnyanyasaji' Netanyahu
Erdogan aadhimisha Eid al-Adha kwa ujumbe wa umoja Gaza, amkashifu "muuaji" Netanyahu
Israel inaendelea na uvamizi na mauaji Gaza na Lebanon licha ya makubaliano ya kusitisha mapigano
Uturuki na nchi nyengine 7 zalaani udhalilishaji wa Israel dhidi ya wanaharakati wa Flotilla
Wataalamu wanakusanyika katika Jukwaa la Afrika 2026 ili kujadili uhusiano kati ya Uturuki na Afrika
Idara ya Ujasusi ya Uturuki yanasa washukiwa 10 wa Daesh katika operesheni ya Syria
Uturuki imekuwa kitovu cha nishati, mtetezi wa amani huku kukiwa na mvutano wa kikanda: Rais Erdogan
Erdogan wa Uturuki asisitiza kuunga mkono uhuru wa Sudan katika mazungumzo na Waziri Mkuu Idris
Rais Erdogan wa Uturuki amlaki Waziri Mkuu wa Sudan jijini Ankara
Rais Erdogan amwambia von der Leyen kuwa mvutano wa kikanda unahitaji uhusiano wa Uturuki na EU
Waturuki walio diaspora ni muhimu kwa ushawishi unaokua wa Uturuki duniani, anasema balozi
Uchokozi' wa Israel lazima ukomeshwe kwa amani ya Mashariki ya Kati: Rais wa Uturuki Erdogan
Erdogan atoa wito wa ushirikiano kati ya nchi za Turkic katika ulinzi, AI na usalama wa mtandao