Walid Regragui ajiuzulu ukocha Morocco
Walid Regragui amejiuzulu wadhifa wake wa kocha mkuu wa Morocco miezi michache baada ya kuwaongoza Simba wa Milima ya Atlas katika fainali ya AFCON 2025 nyumbani.
Regragui mwenye umri wa miaka 50 pia aliisaidia timu hiyo ya Afrika Kaskazini kutinga katika Kombe la Dunia la 2022 nchini Qatar na kuweka historia kama nchi ya kwanza kutoka Afrika kufika hatua hiyo ya nne bora.
Kocha wa timu ya Olimpiki ya Morocco Mohamed Ouahbi, atachukua nafasi ya Regragui na atainoa kwa ajili ya Kombe la Dunia nchini Marekani, Mexico na Canada.
“Haya siyo mabadiliko tu ya kawaida. Lengo ni kuhakikisha maendeleo ya soka la Morocco kupitia utaratibu maalum.”
Morocco inaanza mechi zake za hatua ya makundi dhidi ya mabingwa mara tano wa Kombe la Dunia Brazil tarehe 13 Juni kabla ya kukipiga dhidi ya Scotland na Haiti katika kundi C.
Simba hao wa Milima ya Atlas wanapambana na Ecuador na Paraguay katika mechi za kimataifa za kirafiki.