| Swahili
UTURUKI
1 dk kusoma
Rais Erdogan atadhaharisha mfumo wa baada ya Vita ya Pili ya Dunia kupoteza uhalali wake
Kulingana na Rais Recep Tayyip Erdogan wa Uturuki, mifumo mbalimbali iliyoanzishwa baada ya Vita Kuu ya Pili ya Dunia inapoteza uhalali wake.
Rais Erdogan atadhaharisha mfumo wa baada ya Vita ya Pili ya Dunia kupoteza uhalali wake
Ujumbe kwa njia ya video wa Rais Recep Tayyip Erdogan wa Uturuki./Picha:AA
27 Machi 2026

Mifumo iliyoanzishwa na mataifa washindi wa Vita Kuu ya Pili ya Dunia, huenda ikapoteza uhalali wake, rais wa Uturuki alitahadharisha siku ya Ijumaa.

"Taasisi na kanuni za mifumo hiyo inaonekana kukosa kazi,” alisema Erdogan kupitia ujumbe wa video uliotumwa wakati wa mkutano wa Stratcom uliofanyika jijini Istanbul.

"Ulimwengu unapitia kipindi kigumu kilichotawaliwa na mauaji ya kimbari, vita na huzuni ambapo kuna vita ya nishati, teknolojia na biashara huku mizozo ikitatuliwa kupitia mapigano badala ya mazungumzo."

"Hakuna kitu cha muhimu kwa wakati huu kama kumaliza majanga yanayaoendelea Gaza na kurejesha amani na utulivu duniani," alisema Erdogan.

Aligusia umuhimu wa kuimarisha mawasiliano na ushirikiano katika kukabiliana na usambaaji wa taarifa potofu, akizitaka serikali na taasisi za wasomi kuchukua hatua madhubuti.

"Uturuki itaendelea kushikilia msimamo wake wa kupambania amani na utulivu duniani," aliongeza.

 

 

CHANZO:AA