| Swahili
AFRIKA
1 dk kusoma
Uchochezi wampeleka Tundu Lissu jela miaka minne
Hata hivyo, mwanasiasa huyo alipinga uamuzi wa mahakama wa kumtia hatiani kwa kosa la uchochezi, akieleza kuwa tangu mwanzo alikuwa akikabiliwa na shtaka la uhaini na si kosa hilo ambalo mahakama imemtia hatiani.
Uchochezi wampeleka Tundu Lissu jela miaka minne
Mwanasiasa huyo alipinga uamuzi wa mahakama wa kumtia hatiani kwa kosa la uchochezi.

Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala Ndogo ya Dar es Salaam imemhukumu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Antipas Lissu, kifungo cha miaka minne baada ya kumkuta na hatia ya uchochezi.

Hukumu hiyo Novemba 6, 2026, na jopo la majaji watatu lililoongozwa na Jaji Dunstan Ndunguru, huku majaji wengine wakiwa James Karayemaha na Ferdinand Kiwonde.

Katika uamuzi wake wa awali, mahakama ilimuachia huru Lissu katika shtaka la uhaini baada ya kubaini kuwa upande wa mashtaka haukuthibitisha viini muhimu vya kosa hilo, lakini ikamkuta na hatia ya kosa dogo la uchochezi.

Kabla ya kutolewa kwa adhabu hiyo, Lissu alipewa nafasi ya kuzungumza mbele ya mahakama, ambapo alisisitiza kuwa hana sababu ya kuomba msamaha kwa kuwa anaamini hakutenda kosa lolote.

Mwanasiasa huyo alipinga uamuzi wa mahakama wa kumtia hatiani kwa kosa la uchochezi, akieleza kuwa tangu mwanzo alikuwa akikabiliwa na shtaka la uhaini na si kosa hilo ambalo mahakama imemtia hatiani.

Pia, alidai kuelezwa kuwa ameelezwa kuwa ana haki ya kukata rufaa kupinga uamuzi huo kwa mujibu wa taratibu za kisheria.

CHANZO:TRT Afrika Swahili